'Hawana pesa ya kununua kondomu,'Akothee awashambulia wanaume wanaommezea mate

Kupitia kwenye ukurasa wake wa facebook Akothee amewaonya wanaume ambao wanamuonea wivu kwa ajili ana mpenzi wake Omosh.

Muhtasari
  • Msanii huyo aliendelea na kuwaambia kwamba amechoka kuwapa block kwa hivyo wanaweza kuacha kumfuatilia mitandaoni
Akothee na mpenzi wake

Ni mwanamume yupi ambaye amemchokoza au kummezea mate msanii maarufu Akothee?

Kupitia kwenye ukurasa wake wa facebook Akothee amewaonya wanaume ambao wanamuonea wivu kwa ajili ana mpenzi wake Omosh.

Msanii huyo aliendelea na kuwaambia kwamba amechoka kuwapa block kwa hivyo wanaweza kuacha kumfuatilia mitandaoni.

"Baadhi ya wanaume hapa wana uchungu tangu wakati Omosh alijitokeza, kwani mlikuwa na matumaini mtakuwa Ukiwa umepitia bundles na Dm sijibu Aiii hii imewaumaa sanaa , Na ngoha mwaka ujao mjipange kuhama hii ukurasa huu na muache kunifuata mitandaoni kwani nimechoka kuwapa block wacheni kunifuata kwa amani yenu kwanini uwe kwenye ukurasa wa mtu ambaye alingani na akili yako? ni wewe unanifuata ,sina wazo nini unachofuata nampenda Mr Omosh anawaonyesha wanaumejinsi mwanamke anapswa kulindwa Ona sasa najengewa,"Aliandika Akothee.

Huku akijibu shabiki aliyewakemea wanaume kama hao, Akothee aliwakema na kuwasuta wanaume huku akisema hawana hata pesa ya kununua kondomu.

"Hawana hata pesa za condoms ,ni wewe umeze P2 this men of nowadays so useless," Aliandika Akothee.