Alikuwa amelewa-Willy Paul aweka mambo bayana baada ya Jovial kudai si mpenzi wake

Kwa hivyo, ukaribu huo uliofichwa ulikusudiwa kuvuta hisia za mashabiki wao walipotoa wimbo mpya uliopewa jina La la la.

Muhtasari
  • Alisema kuwa Willy Paul na yeye walikuwa wanafanya kazi kwenye mradi ambao walimaliza na kuachana
Willy Paul na Jovial
Image: Wily Paul Instagram

Msanii Jovial amevuma sana mitandaoni baada ya kudai kwamba yeye sio mpenzi wake msanii Willy Paul.

 Sababu zake ni kwamba hakuweza kustahimili joto kichwani kutoka kwa mashabiki tena.

Alisema kuwa Willy Paul na yeye walikuwa wanafanya kazi kwenye mradi ambao walimaliza na kuachana.

Kwa hivyo, ukaribu huo uliofichwa ulikusudiwa kuvuta hisia za mashabiki wao walipotoa wimbo mpya uliopewa jina La la la.

Hata hivyo ametaja kuwa wote wawili walinufaika kutokana na kile walichokifanya, jambo ambalo lilifanya mitandao ya kijamii kuwa mbaya

"Pooze sio mwanamume wangu, ni rafiki yangu ilikuwa biashara na tunufiaka sisi sote, sasa turudi kwenye ukweli, naumia nimeshindwa kuvumilia 

Mungu nisaidie kwa yatakyo fwata, mayooo," Jovial Aliandika.

Huku Willy Paul akijibu madai ya Jovial alisema kwamba alikuwa amelewa na kwamba msanii huyo ni mpenzi wake.

"Tafadhali msitilia maanani uvumi huo, alikuwa amelewa aliposema hayo.. @jovial_ke mambo ya nyumbani tumalize nyumbani please 🙏,"Alisema Willy Paul.