Niliwahi haribikiwa na mimba mara 3-Hamisa Mobetto afichua

"Sidhani kama nimewahi kumuomba mtu yeyote msaada wa kulea watoto wangu.

Muhtasari
  • Mobetto aliwaambia watu wamzungumzie yeye iwapo wana jambo linalowatatiza kumhusu ila wasimhusishe mwanawe
Image: INSTAGRAM// HAMISA MOBETTO

Mwanasosholaiti Hamisa Mobetto aiwa kwenye mahojiano, amefichua kwa mara ya kwanza kwamba amewahi haribikiwa na mimba kabla ya kumzaa mwanawe Dylan.

Akiwa na hisia alifichua kuwa kabla ya kushika mimba ya Dee Dylan aliwahi kuharibikiwa na mimba kadhaa ambazo zilifikia tatu na walikuwa na jitihada nyingi na diamond kumpata mtoto huyo ambaye watu wanamtuhumu kuwa si mtoto wake Diamond.

"Kama kuna mtu alikuwa na uhakika wa Dylan ni Diamond mwenyewe,kabla ya kumzaa Dylan nilikuwahi pata ujauzito mara tatu."

Aliwaomba watu kukoma kumhusisha Dylan kwa mambo yake kwani hawajawahi kukutana naye.

Mobetto aliwaambia watu wamzungumzie yeye iwapo wana jambo linalowatatiza kumhusu ila wasimhusishe mwanawe.

"Sidhani kama nimewahi kumuomba mtu yeyote msaada wa kulea watoto wangu. Sipendi kero na mtu na mimi si mtu wa kuropoka, chonde chonde tusije onana wabaya.Yaani mmekosa vya kuongea au ni nini?" mwanamuziki huyo alisema.

"Yaani mtoto wangu nyie ndo mumpangie baba?Nyie kama nani haswa?! Binadamu mnapenda sana kujipa mamlaka kwenye maisha ya watu wasiowahusu!" aliendelea.