Udaku ni kitu mbaya',King Kaka ajibu madai ya kufunga harusi na mkewe Nana Owiti

Hata hivo Kaka amejibu uvumi huo na kusema kwamba habari hizo ni udaku tu.

Muhtasari
  • Kupitia kwenye video hiyo Nana alionekana amevalia rinda la harusi huku Kaka akiwa amevalia koti jeupe na suruali nyeusi
Image: INSTAGRAM// KING KAKA

Msanii maarufu King Kaka kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram amewakashifu wanamitandao ambao wanaeneza uvumi kuwa amemuoa au kufanya harusi na mkewe Nana Owiti.

Uvumi huo ulienea mitandaoni baada ya mwanamitandao mmoja kushiriki video ya King Kaka na mkewe wakiwa Diani beach.

Kupitia kwenye video hiyo Nana alionekana amevalia rinda la harusi huku Kaka akiwa amevalia koti jeupe na suruali nyeusi.

Uvumi huo ulizidi baada ya Nana kupakia picha akiwa amevalia pete na kusem kuwa.

"Ni wakati."

Wakati huo wapenzi hao wawili hawakupakia chochoe kudhibitisha kuwa wamefunga ndoa au la.

Hata hivo Kaka amejibu uvumi huo na kusema kwamba habari hizo ni udaku tu.

"Udaku ni kitu mbaya sana,"Kaka aliandika.

Wawili hao wamekkuwa pamoja kwa zaidi ya miaka 10, na wamekuwa wanandoa maarufu wenye mfano mwema kwa mashabiki na wanamitandao.