Khadija afichua kwa nini hamtambui Diamond kama mkwe wake

Mwimbaji huyo nguli wa Taaarab alikanusha zaidi madai kuwa ndoa ya siri kati ya Zuchu na Diamond ilifanyika.

Muhtasari
  • “Hii ni habari kwangu. Si kweli, binti yangu hajaolewa wala hajanitambulisha kwa mtu yeyote kwa ajili ya ndoa,” Mama Zuchu aliongeza
Khadija azungumzia suala la bintiye Zuhura kuolewa
Khadija azungumzia suala la bintiye Zuhura kuolewa
Image: HISANI

Mama mzazi wa mwimbaji wa Bongo Flava Zuchu, Khadija Omar Abdallah Kopa amefichua kuwa bintiye hajaolewa licha ya taarifa kuwa Zuchu anamchumbia bosi wake Diamond Platnumz.

Khadija Kopa katika mahojiano yake na Mbego TV, alisema bintiye bado hajamtambulisha rasmi kwa mtu yeyote, na kuongeza kuwa anatarajia mwanaume yeyote, si Diamond pekee.

"Zuhra ni mwanamke, ikiwa kuna mwanaume anataka kumuoa na ambaye yuko tayari na sio Diamond peke yake, basi mimi sina suala, nataka mkwe," Kopa alisema.

Mwimbaji huyo nguli wa Taaarab alikanusha zaidi madai kuwa ndoa ya siri kati ya Zuchu na Diamond ilifanyika.

“Hii ni habari kwangu. Si kweli, binti yangu hajaolewa wala hajanitambulisha kwa mtu yeyote kwa ajili ya ndoa,” Mama Zuchu aliongeza.

Hata hivyo, hisia za Khadija Kopa zilitofautiana na zile za mamake Diamond, Mama Dangote, ambaye ameuchukulia uhusiano wa mwanawe na Zuchu kwa njia tofauti.

Hii ilionekana wakati wa siku ya kuzaliwa ya Zuchu alipomtumia matakwa akimtaja kama binti-mkwe wake.

"Nakutakia maisha marefu yaliyojaa baraka binti mkwe Zuhura Othman Soud," Mama Dangote alisema.