Justina Syokau amenivunja moyo-Mcheshi Consumator alia

Alidaiwa kumnunulia gari mpya aina ya BMW X5 kama pendekezo la ndoa.

Muhtasari
  • Mchekeshaji huyo amesema kwamba amevunjika moyo na sasa ameamua kufunga ukurasa huo
Mwanamuziki wa nyimbo za injili Justina Syokau
Mwanamuziki wa nyimbo za injili Justina Syokau
Image: HISANI

Mmoja wa wacheshi maarufu wa Kenya na pia mtayarishaji maudhui Consumator hatimaye ameamua kuzungumza baada ya mpenzi wake wa muda mrefu, Justina Syokau kudaiwa kupewa zawadi ya gari jipya aina ya Landcruiser V8 Yenye Thamani ya ksh. Milioni 20.

Hata hivyo kulingana na wanamitandao wengi V8 inaonekana kutumika kupita kiasi.

Mchekeshaji huyo amesema kwamba amevunjika moyo na sasa ameamua kufunga ukurasa huo.  

Alidaiwa kumnunulia gari mpya aina ya BMW X5 kama pendekezo la ndoa.

Mchekeshaji huyo amesema hadharani kwamba anapanga kumpa zawadi ya gari msichana mnyenyekevu kama Pritty Vishy.

Consumator amewasiliana na Justina Syokau mara kadhaa, lakini Justina alikataa ombi lake.

"Naskia Justina syokau amepatiwa gari by another guy. So she refused my genuine car. Can't believe it. Am heartbroken. I have decided to close that chapter. Afadhali hata nipatie hii BMWX5 nilikuwa nimemnunulia kwa msichana humble kama Pritty Vishy,"Alisema Consumator.

Hta baada ya wanamitandao kudai kuwa gari alilozawadiwa Syokau limetumika,msanii huyo wa nyimbo za injili alijitetea na kuwashauri wana mitandao wamuache afurahie maisha yake.