Bahati hatimaye afichua kwa nini alitoweka na kunyamaza baada ya kushindwa uchaguzi

Mwimbaji huyo alipoteza uchaguzi huyo kwa mgombea wa ODM Anthony Oluoch.

Muhtasari

•Mwimbaji huyo ameweka wazi kwamba alichukua mapumziko kutoka kwa umma ili kuangazia muziki wake.

•Alibainisha kuwa ilikuwa ni mapumziko ya mitandao ya kijamii ya kwanza aliyokuwa akichukua katika kipindi cha miaka kumi

Kevin Bahati,akihutubia wanahabari siku ya JUmatatu Aprili/25/2022 katika hoteli ya Luke Nairobi
Image: WILFRED NYANGARESI

Mwanamuziki mashuhuri Kelvin Kioko almaarufu Bahati hatimaye amefunguka kuhusu ukimya wake punde baada ya uchaguzi wa Agosti 9, 2022.

Mwaka jana, msanii huyo mwenye umri wa miaka 30 alijitosa katika siasa na alikuwa mmoja wa wagombea kiti cha ubunge wa Mathare akiwania kwa tikiti ya chama cha Jubilee. Hata hivyo, alipoteza uchaguzi huyo kwa  mgombea wa ODM Anthony Oluoch.

Baada ya uchaguzi huo, Bahati alitoweka kwenye vyombo vya habari na mitandao yote ya kijamii huku Wakenya wengi wakikisia kuwa alikuwa amekumbwa na msongo wa mawazo kwa  kutofanikiwa kupata ushindi katika uchaguzi.

Mwanamuziki huyo hata hivyo ameweka wazi kwamba alichukua mapumziko kutoka kwa umma ili kuangazia muziki wake.

"Nilikuwa nimejifungia  tu kwenye Studio ya Nyumbani nikitengeneza Sauti Bora za Muziki kwa ajili yenu mashabiki wangu tangu siku ya kwanza," alisema kupitia ukuraa wake wa mtandao wa nstagram.

Alibainisha kuwa ilikuwa ni mapumziko ya mitandao ya kijamii ya kwanza aliyokuwa akichukua katika kipindi cha miaka kumi

"Naapa nasikiliza nyimbo ambazo nimepanga kuachia mwaka huu wa 2023 ata sina usingizi. Walai sikujua Bahati ni mkali hivii," alijigamba.

Bahati alidokeza kuwa umahiri wake katika muziki umeongezeka huku akifanya mzaha kuwa huenda imechangiwa na kuibiwa kwa kura zake.

Katika uchaguzi wa mwaka jana, Bahati aliibuka wa tatu katika kinyang’anyiro cha ubunge wa Mathare huku  Anthony Oluoch wa ODM akichukua ushindi. Billian Ojiwa ambaye aliwania kwa tiketi ya UDA alimaliza katika nafasi ya pili.

Hilo lilikuwa ni jaribio la Bahati la kwanza kuwania kiti cha kisiasa nchini Kenya.

Baada ya kuvunjwa moyo katika uchaguzi huo uliokuwa na ushindani mkubwa, mwanamuziki huyo alizama kwenye ukimya mrefu.

Hatimaye aliibuka tena hadharani baada ya takriban miezi miwili kwa wimbo  'Mambo ya Mhesh’ ambao alipakia kwenye YouTube.