Kajala adaiwa kutoka kimapenzi na Msenegali wakati bado akichumbiana na Harmonize

Juma amedai kwamba Kajala tayari amerudiana na mpenziwe Msenegali ambaye hakutambulisha.

Muhtasari

•Juma amedai kuwa Kajala bado alikuwa akichumbiana na Msenegali huyo hata alipokuwa kwenye mahusiano na Staa huyo wa Bongo.

•Juma alidai kwamba raia huyo wa Senegal ndiye aliyemfungulia duka la mavazi bintiye Kajala, Paula Paul.

Image: INSTAGRAM// KAJALA MASANJA

Muigizaji wa filamu Bongo, Frida Kajala Masanja anachumbiana na bwenyenye Msenegali, mtangazaji maarufu Juma Lokole amedai.

Juma ambaye anadai karejesha uhusiano mzuri na mpenzi huyo wa zamani wa Harmonize ameibua madai kuwa bado alikuwa akichumbiana na Msenegali huyo hata alipokuwa kwenye mahusiano na Staa huyo wa Bongo.

Katika mahojiano na Carrymastory, mtangazaji huyo alibainisha kuwa Kajala hajavunjika moyo baada ya kuachana na Harmonize kwani tayari amerudiana na mpenzi wake Msenegali ambaye hakutambulisha.

"Siku zote amekuwa na huyo Msenegali. Hapa alikuwa anatafuta jina," Juma alisema.

Juma alidai kwamba raia huyo wa Senegal ndiye aliyemfungulia duka la mavazi bintiye Kajala, Paula Paul.

"Msenegali huyo ndiye alikuwa anamsomesha Paula, bado anaendelea. Sasa anampeleka Dubai kusomea mambo ya Uhudumu wa ndege. Juzi Paula alikuwa Dubai kutafuta vyuo. Mwezi wa pili anaenda kule," alidai.

Mtangazaji huyo alidai kuwa Msenegali huyo hakuwahi kujua kuhusu uhusiano wa hivi majuzi wa Kajala na Harmonize kwa vile hayupo sana kwenye mitandao ya kijamii. Alisema kuwa muigizaji huyo alikuwa akimdanganya mpenzi huyo wake kwamba anaigiza tu na kuitangaza nchi yake ya Tanzania.

"Ni mtu mwenye akili heshima zake na hela zake, hababaiki na vitu vidogo vidogo vya watoto," alisema Lokole.

Kajala alithibitisha kutengana na Harmonize mwishoni mwa mwaka jana baada ya kuwa kwenye mahusiano kwa takriban miezi saba. Wawili hao waliwahi kuchumbiana tena mwaka wa 2021 kabla ya utengano mbaya.

Mimi kama mwanamke na binadamu nimeumbwa kupenda na kusamehe pia, ila kwenye hili nastahili kuchekwa, nastahili kubezwa na kudharauliwa pia. Sipo hapa kujitetea wala kutia huruma ni kweli nilifanya makosa na nimeyagundua makosa yangu, mimi siyo mkamilifu," Kajala alisema mwezi Desemba.

Aliendelea kufichua kwamba tayari amemsamehe bosi huyo wa Kondegang na kusema yuko tayari kupiga hatua nyingine.

Juma pia alijibu kuhusu madai ya kumuiga Kajala baada ya kununua gari aina ya Range Rover na kuweka nambari ya usajili LOKOLE 1.

Aliweka wazi kuwa hayumbishwi na madai hayo kwani huo ni ushindani mzuri kwa kuwa hakumuumiza mtu yeyote.