Stivo azungumza kuhusu marehemu babake, jinsi familia inavyokabiliana na kifo chake

Stivo alisema mama yake anakubali msiba huo polepole.

Muhtasari

•Simple Boy alisema ni bahati mbaya kwamba marehemu hakufurahia sana mafanikio ya mwanawe.

•Stivo alisema tarehe ya maziko itajulikana baadaye.

Stivo Simple Boy
Image: HISANI

Stivo Simple Boy amemtaja babake marehemu Anthony Adera kama mtu aliyeunga mkono talanta yake.

Akizungumza na Word Is, Simple Boy alisema ni bahati mbaya kwamba marehemu hakufurahia sana mafanikio ya mwanawe.

"Baba yangu hakuwa mgonjwa, alipumzika kwa amani. Hatujafanya uchunguzi wa maiti kujua ni nini kilimuua," alisema.

Stivo alisema mama yake anakubali msiba huo polepole.

"Amekuwa dhaifu sana lakini tunamsaidia. Naomba mashabiki wangu wanisaidie ili nimpe baba yangu mazishi yanayostahili. Bajeti ni Sh400k," alisema.

Alisema tarehe ya maziko itajulikana baadaye. Habari za kifo cha babake zilitangazwa na wasimamizi wake.

Sivo pia aliwaomba mashabiki wake kumuombea yeye na familia yake katika kipindi hiki kigumu.

“Nawashukuru mashabiki wangu kwa kuniunga mkono muda wote huu,” alisema.