Shakilla ajiunga na App ya kuchumbiana katika harakati za kujitafutia mwanamume

“Lazima nitafute mwanamume kwa vyovyote vile” aliandika Shakilla.

Muhtasari
  • Ufichuzi huo hata hivyo unajiri takriban wiki mbili baada ya Shakilla kutumia akaunti yake ya Instagram kutangaza masikitiko yake
Shakilla
Image: INSTAGRAM

Mwanasosholaiti mwenye utata Shakilla  leo amefichua kwa mashabiki wake kwamba amejiunga rasmi na programu ya kuchumbiana ya Tinder.

Alifichua haya kupitia kwenye insta stories zake, ambapo alisema kuwa lengo lake kuu lilikuwa hatimaye kujipatia mwanamume ambaye anatumai atakuwa kwenye uhusiano naye.

“Lazima nitafute mwanamume kwa vyovyote vile” aliandika Shakilla.

Ufichuzi huo hata hivyo unajiri takriban wiki mbili baada ya Shakilla kutumia akaunti yake ya Instagram kutangaza masikitiko yake.

Hii ni kwa sababu hakuna hata mmoja wa wafuasi wake wa kiume kwenye mitandao ya kijamii aliyeonyesha nia ya kutaka kuchumbiana naye.

Kupitia hadithi zake za insta, msichana huyo wa miaka 22 alilalamika kwamba hakuna mwanamume aliyemkaribia kwa uhusiano wa dhati.

Shakilla alizidi kujiuliza kama alikusudiwa kuwa single milele.

"Wafuasi wangu wote hakuna anayetaka kuingia katika uhusiano wa dhati nami. Je, nilikusudiwa kuwa mtaani maishani" Shakilla aliandika.

Aidha mwanasosholaiyti huyo alikiri kwamba hawezi chumbiana na wanaume Wakenya.

"Wanigeria ndio watu watamu zaidi unaoweza kukutana nao wanakupa pesa na kukutendea vyema. Siwezi kamwe kuchumbiana na mvulana Mkenya. Mimi si Mkenya kwa hivyo nina haki ya kufanya hivyo," Shakilla alisema wakati wa kipindi cha moja kwa moja cha Instagram.