Mchumba wa Linet Toto adaiwa kuwa na familia nyingine (+screenshots)

Inadaiwa Kim alikuwa kwenye ndoa na mwalimu na walikuwa na watoto watatu naye.

Muhtasari

•Machapisho ya Facebook ya Kimutai akidaiwa kukiri kuwa na watoto yameibuka kwenye mitandao ya kijami.

•Katika moja ya machapisho yake wakati wa kampeni mnamo Julai 2022, Kim alichapisha kwenye Facebook kwamba alikuwa akiombea ushindi.

Linet Toto achumbiwa
Image: HISANI

Inadaiwa kuwa mchumba wa mwakilishi wa Wanawake wa Kaunti ya Bomet Linet Toto, Godfrey Kimutai almaarufu Nifty Kim alikuwa kwenye ndoa nyingine na hata ana watoto.

Haya ni kulingana na ripoti za mitandao ya kijamii zilizosambazwa baada ya Kimutai kumvisha pete ya uchumba mwanasiasa huyo mdogo mnamo siku ya wapendanao.

Machapisho ya Facebook ya Kimutai akidaiwa kukiri kuwa na watoto yameibuka kwenye mitandao ya kijamii. Picha za skrini zilizoibuka ni kutoka kwa chapisho ambalo inadaiwa alitoa maoni yake miaka 8 iliyopita.

Kulingana na mtumiaji wa mtandao wa kijamii aliyetambulika kwa jina la Rotich Generali, Kim alikuwa kwenye ndoa na mwalimu na walikuwa na watoto watatu naye.

"Mke wa Kim bado yuko katika mshtuko kuhusu mumewe. Anashangaa kwamba alipokuwa shuleni akifundisha, Kim alimdanganya kwamba alikuwa akisafiri kuenda Nairobi kwa mahojiano. Ila akamuona tu akimchumbia Linet...," aliandika.

Akimjibu mmoja wa mashabiki aliyeuliza kama watoto hao ni wake, Kim alisema:

"Ndiyo, ni watoto wangu wa kupendeza na nilikuwa nimewapeleka kwenye ziara ya msitu wa Mau."

Shabiki mwingine alimuuliza kuhusu walipo mama wa watoto hao na Kim akamwambia:

"Usiniulize kuhusu mama yao."

Akizungumzia mmoja wa wanawe, Kim alisema atakuwa meneja kama yeye. "... bila shaka, kama baba yake, atakuwa meneja nadhani."

Walakini, katika moja ya machapisho yake wakati wa kampeni mnamo Julai 2022, Kim alichapisha kwenye Facebook kwamba alikuwa akiombea ushindi.

"Ninaombea ushindi wake, pamoja naye au bila mimi. Nataka kumuona akiwa juu." ikifuatiwa na emoji ya mapenzi.

Radio Jambo ilimpigia simu Mwakilishi wa Wanawake wa Bomet lakini hakujibU. Toto alimtaja mchumba wake kuwa mmoja kati ya milioni moja baada ya kumchumbia.

"Na hatimaye nikasema NDIYO... Kheri ya siku ya wapendanoa mpenzi... Hongera, wewe ni mmoja kati mamilioni, Mungu awe nasi katika safari hii. Nakupenda," aliandika.

Linet aliendelea kuahidi kuwa mtu wa ajabu ambaye anaweza kumfanya bae wake kucheka na kuona ulimwengu pamoja naye.

"Ni sura mpya ya maisha GOLDEN GILDED CAGE ambapo tulifunga pingu za maisha. Shauku kali ya kusahaulika, Kumbukumbu za nyakati za utukufu hazitafifia kamwe. Umeipenyeza nafsi yangu kama labyrinthan. Mapenzi yako yanasikika na kupenyeza udadisi katika pazia na misukosuko upweke wangu katika nguvu...Kuanzia leo hadi mwisho wa wakati, nakukabili kama MFALME wangu katika urafiki wa ajabu wa moyo wangu... Nitafanya siku zako zote zijisikie kama tukio... Matarajio yasiyohesabika na tufanikiwe. ..Na tutembee maili na maili tukiwa tumeshikana mikono. Mungu atubariki."

Utafsiri: Samuel Maina

Image: HISANI
Image: HISANI