Tutaambia nini watu! Wakenya watoa hisia mseto baada ya Karen Nyamu kumposti Samidoh

Karen na Samidoh walihudhuria mazishi ya shemeji wa naibu rais Rigathi Gachagua.

Muhtasari

•Baadaye jioni, Bi Nyamu alichapisha picha kadhaa  za hafla hiyo kwenye kurasa zake mbalimbali za mitandao ya kijamii.

•Wanamitandao wengi waliojibu chapisho hilo walionekana kushangazwa na uchumba wa wawili hao.

wakati wa mazishi ya shemeji ya DP Rigathi Gachagua mnamo Februari 23, 2023.
Seneta Karen Nyamu na Samidoh wakati wa mazishi ya shemeji ya DP Rigathi Gachagua mnamo Februari 23, 2023.
Image: FACEBOOK// KAREN NYAMU

Seneta wa kuteuliwa Karen Nyamu na mzazi mwenzake, Samuel Muchoki almaarufu Samidoh walikuwa miongoni mwa wageni wengi waliohudhuria hafla ya mazishi ya shemeji wa naibu rais Rigathi Gachagua, marehemu Nancy Muthoni katika eneo bunge la Gatanga, kaunti ya Murang'a siku ya Alhamisi.

Baadaye jioni, Bi Nyamu alichapisha picha kadhaa  za hafla hiyo kwenye kurasa zake mbalimbali za mitandao ya kijamii.

Katika taarifa yake, wakili huyo alibainisha kuwa alikuwa amehudhuria ili kufariji familia ya naibu rais.

"Leo nimefariji familia ya naibu rais Rigathi Gachagua kufuatia kifo cha shemeji yake Nancy Muthoni. Alizikwa katika Kijiji cha Kamunyaka, Eneobunge la Gatanga, Kaunti ya Murang'a," aliandika kwenye Facebook.

Kati ya picha alizochapisha ni pamoja na moja ya mzazi mwenzake Samidoh akitoa hotuba yake kwenye hafla hiyo na nyingine inayoonyesha wakiwa wamekaa karibu na kuonekana kufurahia muda pamoja.

Picha hizo zilionekana kuwasisimua sana mamia ya wanamitandao ikizingatiwa kuwa Nyamu alikuwa ametangaza kukatiza uhusiano na mwanamuziki huyo miezi michache iliyopita. Mama huyo wa watoto watatu alichukua hatua hiyo mwezi Disemba baada ya mzozo uliomhusisha yeye, Samidoh na mkewe Samidoh, Edday Nderitu kutimbuka jijini Dubai ambako mwimbaji huyo alikuwa akitumbuiza.

Wanamitandao wengi waliojibu chapisho hilo walionekana kushangazwa na uchumba wa wawili hao.

Eliza Munyaga: Karen Nyamu nafurahia sana kwa ajili yako na yeye, mipango ya kando tuko hapa kuishi.

Seateller Sticulate: Tutaambia nini watu?

_innocencia: Tulikukataza tena umerudi.. tena unampost na hakupost.. haiyaa

jane_lex_liam Sisi wote hatufai kuwahi kusema chochote. Acha tunyamaze daima

kaymoh_20 Mnakaa poa. Naomba Mungu awakumbuke wanawake wote ambao wameolewa kwa sababu ndoa ni ulaghai.

Licha ya Karen Nyamu kuchapisha picha za mzazi mwenza huyo wake, Samidoh hakuchapisha picha ama taarifa yoyote kuhusu hafla hiyo ya Alhamisi.

Wapenzi hao wa zamani pia wanaripotiwa kukutana tena siku chache zilizopita katika kikao na gavana wa Nyandarua Kiarie Badilisha.