Mueni hukuja nyumbani Wikendi-Bahati afunguka kwa nini Mueni aliacha kuishi nao

Mueni angekaa na akina Bahati siku za shule na wikendi aliruhusiwa kwenda kumtembelea mama yake.

Muhtasari
  • Akiongea na Mungai Eve kwenye kituo chake cha YouTube Bahati alifichua sababu kwa nini hatumwoni Mueni tena katika himaya za Bahati

Mengi yamekuwa yakiendelea katika himaya ya Bahati hivi majuzi. Mwaka jana Mueni alijiunga na ndugu zake wa kambo katika shule yao mpya, Juja Preparatory School.

Mueni angekaa na akina Bahati siku za shule na wikendi aliruhusiwa kwenda kumtembelea mama yake.

Shule zilipofunguliwa mapema mwaka huu Mueni hakuwa amerejea katika himaya ya Bahati wala hakuwepo watoto walipokuwa wakinunuliwa sare za shule na vifaa vya kuandikia.

Hii ilipelekea mashabiki wa Bahati na Diana kubashiri kuwa mzozo kati ya baby mamaswa Bahati; Yvette na Diana wanaweza kuwa ndiyo iliyopelekea Mueni kuacha kuishi na akina Bahati.

Akiongea na Mungai Eve kwenye kituo chake cha YouTube Bahati alifichua sababu kwa nini hatumwoni Mueni tena katika himaya za Bahati.

Alisema kuwa mamake Mueni, Yvette Obura aliomba abadilishwe shule ili kuwa na wakati zaidi wa mama na binti.

"Mueni ni binti yangu hiyo haibadiliki. Mueni alibadilisha shule kwa sababu tulikuwa tunakaa na yeye kwa muda mrefu na hakuwa na wakati mwingi wa kushikamana na mama yake. Mama aliomba akue na shule iliyo karibu zaidi. Mama yake aliomba shule karibu na mahali pake ili awe na uhusiano wa karibu na binti yake na ni kiwango sawa na dada. Ninahakikisha wote wanalipa karo sawa za shule."

Bahati hata hivyo alitaja kuwa Mueni huenda kuwatembelea ndugu zake, Morgan, Heaven, Majesty na Malaika wakati wa wikendi.

"Mueni huja nyumbani wikendi. Ilikuwa haki kwa sababu mwisho wa siku anahitaji kuwa na uhusiano wa karibu na mama yake kadri anavyohitaji kuwa na uhusiano na dada zake wengine."

Haya yanajiri siku chache baada ya mashabiki kudai kwamba kuna ugomvi kati ya Diana na Yvette.