Walinitukana bila sababu yeyote-Willy Paul alia baada ya kushambuliwa hadharani

Msanii huyo aidha alisema kwamba wanaume hao walimpata akiwa ameegesha gari lake,na kuchukua video wakimtukana.

Muhtasari
  • Kwa kweli msanii Willy Paul anafahamika sana nchini hata safari ya muziki wake wengi wanahifahamu
Image: INSTAGRAM// WILLY PAUL

Kuwa mtu maarufu,msanii, au mwigiaji nchini,ni jambo ambalo linahitaji umakini ako kwani wengi hupitia mikononi mibaya ya mashabiki wao na wanachi kwa jumla.

Kwa kweli msanii Willy Paul anafahamika sana nchini hata safari ya muziki wake wengi wanahifahamu.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram siku ya Jumamosi msanii huyo alipakia gari lenye namba ya usajili KDA 156 S ambayo alidai kwamba kuna wanaume ambao walimtukana bila sababu yeyote.

Msanii huyo aidha alisema kwamba wanaume hao walimpata akiwa ameegesha gari lake,na kuchukua video wakimtukana.

Kulingana naye hakuwajibisha bali anawasubiri wapakie video hiyo,pia aliwafahamisha kwamba anawafahamu sasa.

"Mwenye gari hili wamenipata nikiwa nimeegesha gari langu kwenye kituo cha mafuta cha Rubis,wakatoa camera wakaanza kurekodi wakinitukan bila sbabu yeyote 

Waliniita majina yote, kwa sababu walijua niko hadharani singefanya chochote,kama anijua basi wajua vizuri sinaga ubaya na mtu,ujumbe wangu kwa watu hawa ni kuwa nina kila kitu kuwahusu kwa hivyo tunasubiri mpakie video hiyo mitandaoni,"Willy Alisema.