Ndoa sio kwapa-Mwijaku ampasha Fridah Kajala baada ya madai Paula amefunga ndoa

Pia alizidi kumpasha aneno makali mwanasosholaiti huyo huku akisema kwamba ndio sio kwapa.

Muhtasari
  • Habari hizo za kustaajabisha zimeshangaza wengi kwani baadhi ya mashabiki wake walikuwa wakimpongeza kwa sura yake mpya zaidi katika Maisha
Image: mwijaku/twitter

Saa chache zilizopita mwanasosholaiti maarufu nchini Tanzania na mwanadada Fridah Kajala amepakia picha za mwanawe Paula Kajala akiwa na mavazi ya harusi.

Kwenye picha Paula amewashangaza mashabiki wake baada ya kutoka na mumewe kwenye mavazi na miundo ya harusi ya kitamaduni ya Kiislamu.

Habari hizo za kustaajabisha zimeshangaza wengi kwani baadhi ya mashabiki wake walikuwa wakimpongeza kwa sura yake mpya zaidi katika Maisha.

Hata hivyo mmoja wa washirika wa karibu wa harmonize ambaye alikuwa baba yake wa kambo kabla ya kuachana na mamake Fridah Kajala ameingia kwenye mitandao ya kijamii na kumpasha Kajala.

Kwenye post yake mtangazaji huyo wa Clouds TV amemchana Kajala akimwambia kuwa Paula bado ni mtoto wa shule na amefanya kosa kubwa sana kumuhusisha na watu waliokomaa mambo kama kumuoa akiwa bado mdogo.

Mwijaku pia ameendelea kusema kuwa huenda asidumu kwenye ndoa hiyo.

"Mikosi mingine mnajitakiaga wenyewe mtoto hata shule hajamaliza una muhusisha na zinaa ya ukubwani . AKIOLEWA na KUDUMU kwenye NDOA uniite NGURUWE PORI nimekaa paleee CMG natangaza Kipindi,"Alisema Mijaku.

Pia alizidi kumpasha aneno makali mwanasosholaiti huyo huku akisema kwamba ndio sio kwapa.

"Namuwaza #VANYBOY na #KONDEBOY wana hali gani ? NDOA SIO KWAPA USEME KILA MTU AIPATE."