Willy Paul:Nilimlipa Zuwena wangu shilingi milioni 2 za Kenya kuwa vixen

Muhtasari

•Willy Paul pia alidai pia kuwa Zuwena aliyemtumia kama vixen ni mrembo mara hamsini zaidi ya ule wa wimbo asili wa Zuwena wake Diamond.

Image: INSTAGRAM// WILLY PAUL

Msanii Willy Paul amedai kuwa alimlipa Zuwena wake shilingi milioni 2 ili kucheza kama vixen kwenye video yake.

Willy Paul aliwasuta wale waliomsuta wakisema kuwa alinakili wazo wa wimbo wake msanii wa Tanzania Diamond Platinumz aliyetoa kibao cha Zuwena mwezi mmoja uliopita.Pozze alisema aliwakejeli kwa kusema shilingi milioni 2 alizomlipa zilikuwa za Kenya na si Tanzania.

"Baada ya kusikiliza kisa cha Zuwena ilibidi nimweke Zuwena huyo huyo kwenye wimbo, sioni shida yoyote ,elewa kwa upole ,si jambo zito"alisema mtanadaoni.

Willy Paul pia alidai pia kuwa Zuwena aliyemtumia kama vixen ni mrembo mara hamsini zaidi ya ule wa wimbo asili wa Zuwena wake Diamond.

"Nilimplipa Zuwena wangu 2 milioni pesa za Kenya ila si za Tanzania,kwa wale waliosema kuwa nimenakili mmeshangazwa semeni sahii niwaonyeshe sura ya Zuwena wangu, ni mrembo mara 50 ya yule mnayemfikiria.Huu ndio mwaka ule"

Willy Paul vile vile alisema kuwa yeye si msanii wa kuchezewa, alidai kuwa yeye ndiye nambari moja bila pingamizi na kuwa hakuna jambo ambalo wasanii wanaweza kumwambia. Aliongezea kuwa kama umeme umewashinda watawezana na yeye ambaye ni injini.

Willy Paul ni msanii wa Kenya ambaye hapo awali alikuwa anaimba nyimbo za injili.