Andrew Kibe afichua mastaa ambao 'wamemblock' kwenye Instagram

Andrew Kibe alidai kuwa wale waliompiga block hawana ufahamu wa burudani na showbiz.

Muhtasari

• Andrew Kibe amejipata katika ugomvi na vita vya mtandao kati yake na baadhi ya mastaa kwa kuwakashifu kwa kile anachodai ni mienendo mibovu.

Marua amjibu Kibe
Marua amjibu Kibe
Image: Instagram

Aliyekuwa mtangazaji wa redio , Andrew Kibe amewataja mastaa ambao wamempa 'block' kwenye Instagram.

Kibe alidai kuwa wale waliompiga block hawana ufahamu wa burudani na showbiz.

Baadhi yao alisema wamemzuia ni pamoja na Pulse Live, aliyekuwa mtangazaji wa radio Kamene Goro, Terence Creative na mke wake Milly.

Kibe alisema hahisi vizuri kwa sababu hakuwa na ubaya ila anajaribu kukosoa tabia zao tu.

Ingawa  ana ugomvi na Diana B, Kibe alisema kuwa Diana hajamblock. Hivi majuzi, Diana B alisema kuwa hana ubaya na Andrew Kibe na kwamba ni burudani tu anafanya.

Bahati na Diana walionekana kutokerwa na kashfa za Andew Kibe kwao kwenye mtandao.

Presenter Ali pia alitajwa kama mtu aliyempiga block Andrew katika mtandao wa Instagram. Kibe alisema kuwa walikosea hivyo basi wakubali kukashifiwa na wapate kujifunza kutokana na kashfa hiyo.

Kibe aliongezea kuwa Jalas hajampiga block kwa sababu yeye anaelewa burudani.

Alitaja NRG radio pia kuwa kama mojawapo ya stesheni na watu waliomblock. Kibe alieleza mshangao wake ni kwanini stesheni aliyoifanyia kazi wamembock kwenye Instagram hivyo akidai aliyesababisha hilo ni Mwalimu Rachel.

Andrew Kibe alieleza kuwa hana jambo zuri wala baya la kusema kuhusu mwalimu Rachel ila atachunguza ili ajue nini kilisababisha hatua hiyo.

Andrew Kibe kwa sasa amejipata katika ugomvi na vita vya mtandao kati yake na baadhi ya mastaa kwa kuwakashifu kwa kile anachodai ni mwenendo mbaya wa maisha.