Dadake Diamond azungumzia mipango ya ndoa baada ya kuota akiwa mke wa tatu

Esma alisema ilimbidi kuamka na kuomba dhidi ya ndoto hiyo.

Muhtasari

•Dadake Diamond Platnumz, Esma Platnumz alikuwa na ndoto kwamba ataolewa tena kama mke wa tatu.

•Miezi kadhaa iliyopita, Esma alisema kwamba amezama kabisa kwenye dimbwi la mahaba na anatarajia kuolewa hivi karibuni.

Diamond na dada yake Esma
Image: INSTAGRAM// ESMA KHAN

Dadake Diamond, Esma Platnumz alikuwa na ndoto kwamba ataolewa tena kama mke wa tatu.

Esma alifunguka kuhusu ndoto hiyo ya  kutisha iliyomtoka jasho kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Alisema ilimbidi kuamka na kuomba dhidi ya ndoto hiyo.

"Nilipata mshtuko lakini nimeomba dhidi ya ndoto hiyo. Ni afadhali kubaki bila kuolewa ikiwa sitapata mwanamume ambaye ni mali yangu pekee," alisema.

Esma aliweka wazi kwamba hatajali kuolewa tena, lakini akasema kwamba ana masharti fulani magumu ambayo mwanaume anayemtaka lazima atimize.

Mwaka wa 2020, mama huyo wa watoto wawili aliolewa kama mke wa tatu na Maulid Msizwa.

Ndoa ya Esma ilidumu miezi mitatu tu baada ya sherehe ya harusi yake ya kifahari.

Miezi kadhaa iliyopita, Esma alisema kwamba amezama kabisa kwenye dimbwi la mahaba na anatarajia kuolewa hivi karibuni.

Alimtaja mwanamume wake kama mwanaume mwenye akili zaidi kuwahi kutokea.

"Yeye ni mchapakazi na ana akili kila wakati na sura yake ni ya kufa," alisema, na kuongeza kuwa yuko tayari kutumia maisha yake yote pamoja.

"Ndoa yangu ijayo haitadumu miezi mitatu kama ile ya awali. Siwezi kuchumbiana na mtu ambaye hawezi kuniinua."