Mume wangu anawakosesha wanaume usingizi, Akothee adokeza

Akothee alisema kuwa hakuolewa na mume wake kwa sababu ya mali.

Muhtasari

•Akothee na Schweizer walifunga ndoa hivi majuzi katika hoteli ya Windsor.

•Akothee alisema kuwa watafanya harusi ya pili katika nchi ya Uswisi Julai mwaka huu.

Akothee na mume wake Denis Shweizer
Image: INSTAGRAM// AKOTHEE

Mjasiriamali na mama wa watoto 5, Esther Akoth almaarufu Akothee amedokeza kuwa mume wake Denis Schweizer anawakosesha wanaume usingizi.

Akothee mbali na hiyo alidai kuwa hawezi kuolewa na mtu asiye na chochote .Aliongezea kuwa ana urembo na uzuri hivyo anawavutia watu kama mume wake Shweizer.

"Siwezi kuolewa na mtu bila,chochote, ingalikuwa hivo ningekuwa niliolewa na hao kitambo,mimi ni mrembo na napendeza ndiposa ninavutia watu kama Omosh," alisema Akothee kupitia Instagram.

Akothee aliongezea kuwa si mali anafuata katika kuolewa kwa sababu amejiendeleza na ana mali zake.

"Siwezi kuolewa kwa sababu ya mali,nina mali zangu. Ingekuwa ni kuhusu suala la mali, nimekataa maombi tatu ya ndoa kutaoka hata kwa bilionea. Ni ngumu kupata mwanamke kama mimi, nliolewa na "Prince Charming' kwa sababu najua thamani yake" alikiri  Akothee.

Mama huyo mwenye miaka 40 aliweka wazi kuwa anafahamu vizuri familia ya mume wake pamoja na mali yake na kwamaba ana kila kitu anachotaka katika mwanaume.

Akothee alisema mbali na mume wake kuwa wa thamani , ana mchezo mwema kitandani. Aliwasutaa wanaompinga akisema kuwa kama Schweizer atakuwa ni sababu ya kifo chake au kuanguka kwake ni sawa mradi wamesoma.a

Akothee na Denis Schweizer walifunga ndoa hivi majuzi kwa harusi ya kifahari iliyofana. Akothee alidai kuwa watafanya harusi ya pili nchini Uswisi. Alidai kuwa kwa sasa anaongoja kumaliza mtihani wake wa shahada ya biashara ili wafunge safari kwenda fungate yao.