Mbunge wa zamani mwenye miaka 80 afunga harusi ya 9 na mrembo wa miaka 27

Ameoa mara nane hapo awali, na amezaa watoto 18. Ndoa zake za awali zimeisha kwa talaka.

Muhtasari

• Picha za ndoa za kitamaduni za wanandoa zinaonyesha jinsi walivyo na furaha wanapochukua hatua hii.

• Tayari wanapanga fungate yao, ambayo itafanyika Ulaya.

Dominic Fobih na mke wake mpya.
Dominic Fobih na mke wake mpya.
Image: Ghana News

Mbunge wa zamani wa nchini Ghana mwenye umri wa miaka 80 ameripotiwa kufunfa harusi yake ya tisa na mrembo mwenye umri wa miaka 27.

Kulingana na taarifa za vyombo vya habari nchini humo, Dominic Fobih alifunga ndoa yake ya 9 na mrembo mnamo Mei 7 mwaka huu.

Harusi ilifanyika katika nyumba ya familia ya bibi harusi katika Mkoa wa Ashanti nchini Ghana.

Fobih alikuwa amevalia nguo ya kitamaduni ya Kente, huku mke wake mpya akiwa amevalia gauni la corset nyeupe na yenye shanga za dhahabu, jariba moja liliripoti.

Picha za ndoa za kitamaduni za wanandoa zinaonyesha jinsi walivyo na furaha wanapochukua hatua hii.

Kulingana na taarifa, Mwanasiasa huyo alikuwa akijawa na majivuno alipokuwa akipiga picha na mke wake mpya, ambaye alionekana kustaajabisha akiwa amevalia gauni lake la harusi.

Fobih ni Waziri wa zamani wa Elimu na mwanachama wa National Democratic Congress (NDC). Aliwahi kuwa mbunge wa Assin Kusini kuanzia 1992 hadi 2000. Pia ni Waziri wa zamani wa Nchi katika Wizara ya Elimu.

Hii ni ndoa ya tisa ya Fobih. Ameoa mara nane hapo awali, na amezaa watoto 18. Ndoa zake za awali zimeisha kwa talaka.

Ndoa ya hivi punde ya Fobih imekumbwa na maoni tofauti kutoka kwa Waghana. Baadhi ya watu wamempongeza kwa kupata mapenzi, huku wengine wakimkosoa kwa kuoa mwanamke ambaye ni mdogo sana kwake.

Bila kujali maoni ya umma, Fobih na mke wake mpya wanaonekana kuwa na furaha sana pamoja. Tayari wanapanga fungate yao, ambayo itafanyika Ulaya.