Kasirika tu kwa mdomo lakini kitu chenye hutumii patiana - mchungaji awashauri kina mama

Mchungaji huyo wa kike aliwaambia kina mama kuwa hata kama waume zao wanawaudhi, ni kawaida lakini hawafai kukasirika hadi kuwanyima raha za chumbani.

Muhtasari

• Yeye [mumeo] hata hataki umuongeleshe, hataki hadithi zako, kwa hiyo wewe [mke] weka hasira zako mahali.

• Kama umeokoka ujue mojawapo ya sehemu ya kuokoka ni kumlinda na kumjali mumewe - mchungaji huyo alisema.

Mchungaji Lydia Kahiga
Mchungaji Lydia Kahiga
Image: Instagram

Mchungaji mmoja wa kike kwa jina Reverend Lydia Kahiga katika mtandao wa TikTok amezua gumzo pevu mitandaoni baada ya video ya mahubiri yake kuenezwa.

Mhubiri huyo katika klipu hiyo alikuwa anahubiri kuhusu wanawake kuwapa heshima waume zao ili kufanikisha ndoa yenye Amani na mustabalai wa muda mrefu wenye tija.

Katika moja ya funzo la kuwaheshimu wanaume katika ndoa, mchungaji Kahiga aliwausia wanawake kutowanyima wanaume wao haki zao za ndoa, sio tu kuwapa heshima bali pia kukubali kushiriki kitendo cha ndoa nao, kwani hiyo ndio moja ya njia chache tu za kuonesha upendo kwa mumeo na kumzuia kutotafuta haki hiyo nje ya ndoa.

Kulingana na mchungaji Kahiga, kila mwanamke anafaa kumpa mumewe ‘kitu’ ambacho yeye hakitumii na si kukikwamilia wakati hakimfaidi kisa amemkasirikia mumewe.

“Mama aokoke kila pahali, Bwana asifiwe sana. Kama umeokoka ujue mojawapo ya sehemu ya kuokoka ni kumlinda na kumjali mumewe. Na unafaa umjali vizuri. Kitu yenye uko nayo na hutumii, mpe mwenye anatumia,” mchungaji huyo aliongea kwa lugha ya mafumbo huku waumini wakishindwa kuzuia vicheko vyao.

“Ni ukweli, hutumii lakini umekwama nayo eti umekasirika,” aliongeza.

Mchungaji huyo alisema kuwa katika ndoa kukasirikiana hutoa aghalabu lakini akatoa ushauri kuwa licha ya kuwepo kukasirikiana, basi wanandoa wanafaa kukasirikiana kwa midomo tu lakini masuala ya chumbani yanafaa kuendelea kama kawaida pasi na kuhitilafiwa kwa njia yoyote.

“Ukikasirika kasirika tu kwa mdomo lakini kitu chenye hutumii patiana. Yeye [mumeo] hata hataki umuongeleshe, hataki hadithi zako, kwa hiyo wewe [mke] weka hasira zako mahali lakini kitu chenye hutumii patiana tafadhali, si chako,” mchungaji huyo alihoji.

Hii hapa video ya mahubiri hayo: