Wasanii maarufu wajitokeza kuonyesha utajiri wao.

Video hizi zimejitokeza mitandaoni baada ya video ya Sonko kuenea.

Muhtasari

• Katika video hiyo, Sonko alionekana ndani ya nyumba yake huku akimfokea vikali kwenye video mtu ambaye anadaiwa kumdhihaki kwamba hana pesa na amefilisika.

• Mchekeshaji Erick Omondi alijitokeza Alhamisi na bashaha tele akiwa na mabunda ya shillingi milioni 13.

Erick Omondi, Oga Obinna na Mulamwah.
Erick Omondi, Oga Obinna na Mulamwah.
Image: INSTAGRAM

Baada ya video ya aliyekuwa gavana wa Nairobi Mike Sonko kuenea mitandaoni akionyesha mabunda ya pesa  baadhi ya wasanii nchini wamejitokeza wakijipga kifua kwa utajiri wao.

Baadhi ya wasanii nchini wamehisi shinikizo na kujitokeza ili kuonyesha utajiri wao. baadhi yao ni pamoja na mchekeshaji Erick Omondi ambaye alijitokeza Alhamisi na bashaha tele akiwa na mabunda ya shillingi milioni 13 huku akionekana kumfokea mtangazaji wa redio Oga Obinna.

“Niko na pesa kukushinda na bado mimi ni mkubwa kukuliko, naeza fungua radio na nikuandike” Erick Omondi alisema kwa kejeli.

Baada ya video ya Erick omodi kuenea, mchekeshaji mwingine David Oyando almaarufu Mulamwah pia akijisifia kua na utajiri mwingi.

Katika video hio Mulamwah anaonekana akikula chakula huku akiwa na mabunda ya pesa mbele yake.

Zaidi ya wachekeshaji hao, mtangazaji wa redio Oga Obinna pia alijitokeza katika akaunti yake ya Instagram na kuchapisha picha iliyoonyesha salio ya shilimgi milioni 53 katika akaunti yake ya benki.  

Katika video hiyo iliyowapa wasanii hawa shinikizo la kutangaza utajiri wao, Sonko alionekana ndani ya nyumba yake huku akimfokea vikali kwenye video mtu ambaye anadaiwa kumdhihaki kwamba hana pesa na amefilisika.

Sonko alionekana akifungua makasha na kuanza kutoa dola za thamani isiyojulikana na muda mfupi baadaye, noti za Kenya, ambazo alisema zilikuwa shilingi milioni mbili.