Mzazi mwenzake Bahati, Yvette Obura ajibu vikali baada ya kuombwa amzalie mtoto mwingine

Yvette na Bahati wana binti mmoja pamoja, Mueni Bahati ambaye sasa ana umri wa miaka saba.

Muhtasari

•Chini ya moja ya machapisho yake, mtumiaji wa Tiktok aliyejitambulisha kama Waithera Salim alimwomba ampe Bahati mtoto mwingine.

•Kauli ya mwanamtandao huyo ilionekana kutomfurahisha Mama Mueni ambaye katika majibu yake alimtaka amzalie msanii huyo mwenyewe.

Image: INSTAGRAM// YVETTE OBURA

Mzazi mwenza wa Bahati, Yvette Obura alijibu kwa kejeli baada ya shabiki kumwomba azae mtoto wa pili na mwimbaji huyo.

Chini ya moja ya machapisho yake, mtumiaji wa Tiktok aliyejitambulisha kama Waithera Salim alimwomba ampe Bahati mtoto mwingine.

"Si upatie Baha second born," Waithera aliandika.

Kauli yake hata hivyo ilionekana kutomfurahisha mama huyo wa binti mmoja ambaye katika majibu yake alimtaka amzalie msanii huyo mwenyewe.

"wee mpatie juu unajua kupeana," alijibu.

Bi Yvette alikuwa amechapisha video ya takriban dakika moja na nusu ambapo alionyesha umbo wa mwili wake mzuri.

Katika video hiyo,  aliuonyesha kwa fahari umbo mzuri wa mwili wake huku akizungukazunguka ndani ya jumba kubwa tupu.

"Video nasibu: Siku katika maisha yangu nikifanya kazi na vyumba vya @home_sweet_home. Asante @_mjukuu kwa video. HELLO HAPPY WEIGHT,” Yvette Obura aliandika chini ya video ambayo alipakia.

Mwili wake mzuri kando, kilichoonekana kuwasisimua wanamitandao ni chaguo lake la wimbo wa kuambatanisha na video aliyochapisha.

Mrembo huyo ambaye ana mtoto mmoja msichana na Bahati anayefahamika kwa jina Mueni Bahati alichagua kutumia wimbo wa mapenzi wa mzazi huyo mwenzake ‘Wanani’ kujigamba kuhusu mwili wake.

"Umeshukia toka binguni. Wee ni malaika. Au Nakosea.Sifa zote tumpee manani., Aliyekuumba hajakose…Toto si toto, uuh lala. Nimeshinda lotto, uuh lala. Figure moto, uuh lala. Toto si toto, uuh lala. Nimeshinda lotto, uuh lala. Kukupata mtoto, uuh lala,” ndio maneno ya wimbo ambao Yvette  alitumia.

Wimbo huo unaendelea, “Basi wewe wanani. Niambie wanani, wanani. Kama sio wangu tuu (x2)…I heard i like you. But i love you. Yes it’s true yes its true.. And if they ask me to choose, Between me and you, Baby i’ll choose you, Cause i’m you uhh uhh..”

Hii huenda ni dokezo nzuri kwamba mfanyibiashara huyo hana kinyongo na mpenzi huyo wake wa zamani na kwamba anashabikia muziki wake.

Katika kipindi cha miezi kadhaa ambayo imepita, Yvette na mkewe Bahati, Diana Marua hata hivyo wamedaiwa kutokuwa na uhusiano mzuri.

Mwezi Machi hata hivyo, Diana alipuuzilia mbali tetesi hizo na kuweka wazi kuwa hana ugomvi wowote na mzazi mwenza huyo wa mumewe.