Kate Actress awajibu mashabiki wanaojulia hali baada ya kutengana na mumewe

Mwigizaji Kate kufurahishwa na jinsi wafuasi wake wanamjulia hali na kuwapongeza.

Muhtasari

• Ujumbe wa Kate Actress kwa mashabiki na wafuasi wanaopiga simu na kutuma jumbe kwenye simu yake baada ya kutengana na Phil ulikuwa shukrani.

• Wapenzi hao wawili walitoa taarifa ya pamoja Jumanne, Septemba 19, 2023, wakisema kwamba ndoa yao ilivunjika muda mfupi uliopita lakini na wakachagua kuweka  mambo yao faragha.

mwigizaji Kate
mwigizaji Kate

  Mwigizaji Catherine Kamau almaarufu Kate Actress ameandika ujumbe wa shukrani kwa mashabiki na wafuasi wake siku chache baada ya kutangaza kutengana na mpenzi wake Phillip Karanja.

Katika ujumbe wake, Kate alitoa shukrani kwa kila mtu ambaye alikuwa amemtumia ujumbe au kumpigia simu kuulizia jinsi anavyoendelea na maisha.

"Asante sana kwa jumbe zenu ninazipokea kila siku  pia jumbe zenye nazipata kila wakati asanteni sana" Kate alisema.

Ujumbe wa shukrani unakuja siku chache baada ya mwigizaji huyo wa zamani wa kipindi  Mother-In-Law kufichua kwamba aliachana na mume wake Phillip Karanja kwa amani.

Phillip Karanja pia alijiunga na mazungumzo hayo kuthibitisha kwamba kwa hakika wametengana  na watu wanapaswa kuwaruhusu waendelee na maisha yao tofauti.

"Hii ni Mambo ya Watu wawili, lakini turuhusu tu iwe hivo ili tuendelee na maisha yetu bila maswali mengi," Phil alisema.

Aliongeza kuwa wanabaki kuwa marafiki; "Mimi na Kate tunabaki kama marafiki, Wazazi wenza na washirika wa biashara,".

Wawili hao walikuwa wameoana kwa zaidi ya miaka mitano sasa na wana binti mmoja pamoja.