Mapenzi tu!: Jamaa atumia Smart TV kuchat na mpenziwe baada ya kunyang'anywa simu (video)

Jamaa huyo alipokonywa simu na mamake wakati akiendelea kuchat na mpenzi wake WhatsApp, alitafuta mbinu mbadala ya kuwasha TV ya kidijitali na kuendeleza gumzo na barafu wa moyo wake.

Muhtasari

• Haraka haraka akatunga ujumbe mfupi, akaongeza emoji ya utani na kubofya tuma, bila kujali ni nani anayeweza kuona mazungumzo yake ya faragha.

• Kwenye kiwambo hicho alionekana alikuwa anachat na mpenzi wake ambaye alikuwa amem’save kwa jina la kimahaba “Bae” pamoja na emoji za mapenzi.

Jamaa akichat kwa kutumia TV.
Jamaa akichat kwa kutumia TV.
Image: TikTok

Jamaa mmoja amewashangaza watu katika mtandao wa TikTok baada ya video kuibuka ikimuonesha akitumia runinga ya kidijitali kuchat na mpenzi wake kwenye program ya WhatsApp.

Video hiyo ilipakiwa na mtumizi kwa jina Enzo Visuals ilionesha kijana mwenye umri wa makamo akiwa amepiga magoti mbele ya runinga kubwa ya kidijitali huku vidole vya mikono yote vikiwa bize kubonyeza kwenye kiwambo chenye herufi kama kwenye simu aina ya kishkwambi.

Kilichowashangaza wengi ni kasi ambayo kijana huyo alikuwa anatumia tena kwa wepesi mno utadhani amezoea kutumia kiwambo cha runinga badala ya kile cha simu.

Haraka haraka akatunga ujumbe mfupi, akaongeza emoji ya utani na kubofya tuma, bila kujali ni nani anayeweza kuona mazungumzo yake ya faragha.

Kwenye kiwambo hicho alionekana alikuwa anachat na mpenzi wake ambaye alikuwa amem’save kwa jina la kimahaba “Bae” pamoja na emoji za mapenzi.

Katika video, mtu huyo aliandika kwamba hiyo ni nadharia ya yule mtu ambaye amepokonywa simu na mama yake lakini bado ni lazima atafute njia mbadala ya kuwasiliana na mpenzi wake.

Klipu hiyo ya kuchekesha imeenea kwenye mtandao wa kijamii, ikiwa na maelfu ya maoni na maoni.

“Mama na baba walichukua rimoti ya tv kumuadhibu mpwa wangu walifika nyumbani na kumkuta anaangalia tv alipakua rimoti kwenye simu yake,” Mmoja kwa jina Desire alisema.

“Sisi wa miaka ya 90 tukituma sms "Nakupenda sana" usijibu ni simu ya mama yangu,” Joe alimwambia.

“TV yangu pia inaunganishwa na WhatsApp kama fr” mwingine alimwambia.

“😅😂Ninahisi kuwa TV pia inaonyeshwa kabla ya asubuhi.” Jodakeed aliongeza.

“MFANO SAFI WA "Nitakwenda mwezini na kurudi kwa ajili yako" Umeliwabo alisema.

“🤣🤣🤣 moyo unataka unavyotaka.” Mwingine alisema.

Maoni yako ni yepi kuhusu video hii?