"Ninakaa sugar mummy?" Mrembo wa miaka 30 akerwa kijana wa miaka 19 kumtongoza (video)

"Ninakaa mwenye pesa kweli, mimi ninaelekea miaka 30, mimi ni mzee sasa. Hata mimi sina pesa, pia natafuta sugar daddy,” aliongeza kwa kero.

Muhtasari

• Mwanamke huyo alishiriki video ya tukio hilo lisilo la kawaida lililotokea kwenye genge la mboga.

• Aliuliza ikiwa yeye anaonekana kama mama wa kuwavizia kimapenzi vijana wadogo kwa kimombo sugar mummy.

Mrembo
Mrembo
Image: X//SCREENGRAB

Mwanamke wa miaka 30 ameonesha kero lake katika mtandao wa X, awali ukiitwa Twitter baada ya kulalamika kwamba katika pitapita zake, mvulana wa miaka 19 alimfuata na kujaribu kumtongoza.

Akishiriki video hiyo, mrembo huyo aliyekwa ndani ya gari lake la kifahari aliuliza watu mitandaoni kwa maoni yao kuhusu ni nini kilichomvutia mvulana huyo mdogo kiumri kumfuata akitaka wawe wapenzi.

Mwanamke huyo alishiriki video ya tukio hilo lisilo la kawaida lililotokea kwenye genge la mboga.

Aliuliza ikiwa yeye anaonekana kama mama wa kuwavizia kimapenzi vijana wadogo kwa kimombo sugar mummy.

Alisema alishangazwa kwamba kijana atakuwa na ujasiri wa kumkaribia kwa uhusiano wa kimapenzi.

“Nina swali moja kwenu wenzangu, je, ninaonekana kama sugar mummy? Kwa sababu sielewi nini kinaendelea siku hizi, nilienda kutafuta chakula cha mchana halafu kuna huyu kijana niko na uhakika ni wa kama miaka 19 hivi, mwembamba na mdogo, alikikaribia na kunisalimia,” Mrembo huyo alianza kueleza katika video.

“Na mimi sikumfokea nilikuwa mkarimu kwake nikamjibu, mambo, unaendelea aje, na akaniuliza kama tunaweza tembea pamoja. Na huyu kijana alinifuata nyuma hadi kwa gari langu na kuniomba namba yangu ya simu. Nini husumbua hawa vijana wadogo? Ninakaa mwenye pesa kweli, mimi ninaelekea miaka 30, mimi ni mzee sasa. Hata mimi sina pesa, pia natafuta sugar daddy,” aliongeza kwa kero.