Ex wangu amenilipa kuhudhuria harusi yake, nifanyeje? - Mrembo aomba ushauri

Mrembo ambaye Ex wake anatarajia kufunga harusi naye ni aliyekuwa rafiki wake wa karibu mno – yaani baada ya kuachana na mpenzi wake, rafiki wake aliingia na kuziba pengo hilo.

Muhtasari

• Yeye, hata hivyo, alisema kwamba alikuwa amesahau kabisa juu yake hadi wakati huo huo alipofanya wadhifa huo.

Tonto Let
Tonto Let
Image: Instagram

Mrembo mmoja ambaye ni mwanasiasa chipukizi na mshawishi katika mitandao ya kijamii amezua mjadala baada ya kujitokeza kuomba ushauri wa cha kufanya kufuatia hatua ya mpenzi wake wa zamani kumpa mwaliko wa kuhudhuria harusi yake – na pia kumlipa ili kufanya hivyo.

Mrembo huyo kutoka Nigeria anayejiita Tonto Let kwenye mtandao wa Instagram aliwataka wafuasi wake kumpa ushauri kuhusu hatua ya kuichukua baada ya mpenzi wake wa zamani kumlipa ili kushuhudia akifunga harusi.

Kinachozua ukanganyifu Zaidi ni kwamba mrembo ambaye Ex wake anatarajia kufunga harusi naye ni aliyekuwa rafiki wake wa karibu mno – yaani baada ya kuachana na mpenzi wake, rafiki wake aliingia na kuziba pengo hilo.

Yeye, hata hivyo, alisema kwamba alikuwa amesahau kabisa juu yake hadi wakati huo huo alipofanya wadhifa huo.

Tonto alionyesha kutoridhishwa kwake na kutokuwa na msaidizi wa kibinafsi na kusema kwamba hakuwa na mavazi ya kuvaa.

“Kusema kweli ninahitaji msaidizi. Ex wangu anafunga harusi na rafiki yangu kesho. Nilikuwa nimesahau kabisa kwa kweli, sina nguo nzuri ya kuvaa. Ninawapenda wote,” Tonto alianza kusema.

Cha kushangaza alionehsa kukubaliana na uamuzi wa Ex wake kuamua kufunga ndoa na mtu mwingine, akisema kwamba anahitaji furaha kama hiyo kwa kile alihisi kwamba nusra alikuwa anamsababishia kuwa chizi.

“Kwa kweli furaha kama hii inamfaa kwa sababu kidogo tu nilikuwa namfanya kuwa mwendawazimu. Kama sitaweza kuhudhuria katika harusi hii nitaonekana na wengi kama Ex mwenye machungu, ikizingatiwa kwamba pia nililipwa ili kuhudhuria, nahitaji vazi,” alimaliza.

Akifafanua Zaidi kwa nini rafiki yake aliamua kuchumbiana na Ex wake, Tonto alisema kwamba wawili hao hawakuanza mahusiano yao wakati yeye akiwa anachumbiana na Ex wake.