Pasta auza kanisa pamoja na waumini wote kwa pasta mwingine na kuhamia ughaibuni

Mchungaji huyo alidaiwa kuwauza waumini, mjengo wa kanisa pamoja na vyombo vyote vya huduma kwa mchungaji mwingine kabla ya kuabiri ndege kwenda nje ya nchi kutafutaunafuu wa kimaisha.

Muhtasari

• Maelezo ya shughuli hii isiyo ya kawaida bado yamegubikwa na siri, na wengi wanashangaa jinsi uuzaji kama huo unaweza kutokea.

• Washiriki wa Kanisa la Graceful Abode walidaiwa kuwa katika mshtuko walipopata habari kuhusu mabadiliko ya ghafla ya uongozi.

Kanisa
Kanisa
Image: BIBLE STUDY TOOLS

Mchungaji mmoja katika Jimbo la Delta nchini Nigeria amekuwa gumzo na kutengeneza vichwa vya habari baada ya kudaiwa kwamba aliuza mjengo wa kanisa lake lakini pia na waumini wote kwa mchunaji mwingine rafiki yake kabla ya kuhamia ughaibuni kutafuta unafuu wa kimaisha.

Kwa mujibu wa toleo la habari, Information Nigeria, mchungaji huyo kwa jina Samwel Ojo, kiongozi wa kiroho kutoka kanisa la Graceful Abode alidaiwa kwamba kabla ya kuondoka Nigeria, alikabidhi kanisa lake na waumini wote pamoja na vyombo vya huduma kwa mchungaji rafiki yake, Michael Ade ambaye alikuwa na kanisa lake dogo eneo ambalo si mbali na eneo la kanisa la Graceful Abode.

Maelezo ya shughuli hii isiyo ya kawaida bado yamegubikwa na siri, na wengi wanashangaa jinsi uuzaji kama huo unaweza kutokea.

Washiriki wa Kanisa la Graceful Abode walidaiwa kuwa katika mshtuko walipopata habari kuhusu mabadiliko ya ghafla ya uongozi.

Matukio hayo hata hivyo yalizua maswali kuhusu maadili na uadilifu wa viongozi wa kidini.

Licha ya hayo, wengine walimuunga mkono mchungaji Samwel kwa kitendo chake cha kuuza kanisa wakisema kwamba alifanya jambo la busara kubadilisha uongozi kabla ya kuondoka kuliko angeondoka na kuliacha kanisa katika mgawanyiko mkubwa waumini wakisalia kupigania vyeo na uongozi pasi na mwelekezi.