Mrembo amzaba kofi la moto mpenzi wake aliyejaribu kumwambia wavunje mahusiano (video)

Wawili hao walikuwa wanabishana mvulana akiweka wazi kwamba uhusiano wao haungeendelea jambo ambalo mrembo alipinga vikali na kumwambia kwamba hakuna kuachana.

Muhtasari

• Video hiyo ambayo imeenea inamuonesha mvulana huyo akimfokea mrembo wake kwamba ameamua kukatisha mahusiano yao.

Mrembo amzaba kofi mpenzi wake
Mrembo amzaba kofi mpenzi wake
Image: Screengrab//X

Kwa kawaida katika mahusiano, mrembo anapoambiwa na mpenzi wake habari za kuvunja uhusiano, aghalabu hulia na kuwa mnyonge.

Lakini kwa mrembo mmoja hai haikuwa hivyo.

Mrembo huyo alikataa kupokea habari za kuachana kutoka kwa mpenzi wake na baada ya mabishano ya muda, alimzaba kofi la moto kwenye shavu akimsisitizia kwamba hakuna kuvunja mahusiano yao.

Video hiyo ambayo imeenea inamuonesha mvulana huyo akimfokea mrembo wake kwamba ameamua kukatisha mahusiano yao.

Licha ya mrembo huyo kuonekana kumbembeleza kutovunja mahusiano, mvulana huyo alionekana kusisitiza kwamba hakuna kitakachoendelea.

Baada ya kumpa makavu, mvulana aliamua kuondoka lakini mrembo alimfuata mbio kwa nyuma na kumshika shati huku akimgeuza kuendeleza kumbembeleza.

Baada ya kuona kwamba hasikii la mwathini wala la mteka maji msikitini, mrembo yule alimzaba kofi mvulana yule na kumwambia usoni kwamba hakuna kuvunja uhusiano wao.

Baada ya kofi la ghafla, watu waliokuwa karibu wakipiga kelele za kustaajabu, huku wengine wakimtetea mrembo kwa kufanya uamuzi wa kumpa kofi la kumfungua akili na kubadili msimamo wake.

Video hiyo ilizua hisia kubwa wakati watoa maoni walipokuwa wakikusanyika kushiriki mawazo yao.

Tazama video ya tukio hilo hapa;