Kipusa kufanya upasuaji kuondoa tumbo la uzazi akisema hataki kuzaa mtoto aje kufa

"Mungu akubariki. Sababu ninafanya upasuaji hivi karibuni ili kutoa tumbo langu. Hakuna mtoto wangu anayekuja katika ulimwengu huu kusubiri kifo,” alichapisha.

Muhtasari

• "Sababu kuu ya kifo ni maisha yenyewe. Kwa hiyo ili kukomesha kifo, ni lazima mtu akomeshe uzazi" alisema.

Mrembo kufanya upasuaji kuondoa tumbo la uzazi
Mrembo kufanya upasuaji kuondoa tumbo la uzazi
Image: X

Mrembo Mwigizaji wa Nollywood, Etinosa Idemudia ametangaza kuwa hivi karibuni atafanyiwa upasuaji wa kutoa tumbo lake la uzazi.

Mama wa mtoto mmoja ambaye alifichua haya muda mfupi baada ya taarifa za ‘uongo’ za kufariki kwa mwanamuziki wa Nigeria Oladips kwenye mitandao ya kijamii alisema, "ili kukomesha kifo, ni lazima kukomesha uzazi."

"Sababu kuu ya kifo ni maisha yenyewe. Kwa hiyo ili kukomesha kifo, ni lazima mtu akomeshe uzazi. Kile ambacho hakijazaliwa hakitakufa kamwe. Hata mimi mwenyewe siko tayari kwa mazungumzo haya ya kina. Ni ya kina kuliko ninavyoweza kuelewa," aliandika kupitia X.

Akijibu maoni ya mtumiaji ambaye alikubaliana naye, Etinosa alisema angetoa tumbo lake, akibainisha kuwa hakuna mtoto wake ambaye atakuja duniani kusubiri kifo.

"Mungu akubariki. Sababu ninafanya upasuaji hivi karibuni ili kutoa tumbo langu. Hakuna mtoto wangu anayekuja katika ulimwengu huu kusubiri kifo,” alichapisha.

Mashabiki wake waligawanyika kwa maoni. Haya hapa ni baadhi ya maoni ya watu;

“Karibu sisi sote tuna maswali kuhusu maisha, kuteseka, kifo, na wakati ujao. Pia tunahangaikia mambo ya kila siku, kama vile kutafuta riziki au kuwa na familia yenye furaha, Maisha yalianzaje? Kwa nini tuko hapa? Kwa nini watu wasio na hatia wanateseka? Nini kinatokea mtu anapokufa?” aliuliza mdau.

“Huu ni uamuzi mzito sana wa kufanya, kumbuka kuwa huu hauwezi kutenduliwa, ukishamaliza ✅,Hakuna kurudi nyuma. Natumai hatajutia maisha haya ya baadaye,” mwingine alisema.

Maoni yako ni yepi?