• Haikutajwa ikiwa kijana huyo kwa jina Benjamin alikuwa akimtania nyanya yake au ikiwa kweli alikuwa na tattoo mkononi mwake
Jamaa mmoja amejipata matatani na nyanya yake baada ya kumtumia picha ya mkono wake kwa simu akitaka kupata maoni yake kuhusu tattoo aliyoichora.
Kijana huyo alipeleka katika mitandao ya kijamii kuomba msaada wa wanamitandao baada ya kufichua kwamba alidhani alikuwa anafanya jambo la busara kumtumia nyanya yake picha ya tattoo lakini hilo limegeuza mambo na sasa anakodolewa na jicho la hatari ya kupata laana na ajuza.
Kijana huyo kupitia mtandao wa WhatsApp baada ya kuchorwa tattoo yenye maandishi ‘God First’ alipiga picha na kumtumia nyanya yake akitaka kujua kama anaikubali.
Hata hivyo, nyanya alicharuka vikali na kusema kwamba kwa tamaduni zao tattoo ni ishara mbaya inayohusishwa na ushirikina na kumtaka kijana huyo kuifuta mara moja la sivyo atampa laana.
Haikutajwa ikiwa kijana huyo kwa jina Benjamin alikuwa akimtania nyanya yake au ikiwa kweli alikuwa na tattoo mkononi mwake.
Video hiyo imepata usikivu kwenye mitandao ya kijamii kwa taswira yake ya kufurahisha ya pengo la kizazi katika mitazamo kuelekea sanaa ya mwili na usemi wa kibinafsi.
Nyanya huyo alimalizia kwa kumwambia kijana huyo kwaheri ya kuonana, akiashiria kwamba tamko lake ndilo lilikuwa la mwisho na halifai kupingwa la sivyo kitakachofuata ni laana tu, basi!
Haya hapa baadhi ya maoni ya watu;
“Nilimtania mama yangu mambo yale yale. Alikaribia kulia kwenye simu.” Mmoja alisema.
“Benjamin ni kama alivuka mstari wa nyanya yake, kimeumana sasa,” mwingine alisema.
Tukio lipi ambalo mzazi au nyanya yako amewahi kulionya vikali dhidi ya kutolifanya?