logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Sijawahi kulipwa kwa kazi ya MC wakati wa uzinduzi wa toroli ya UDA - Anto Neosoul

Jina la chama cha UDA na alama ya toroli ilikuwa sahihi ya Ruto wakati wa kampeni.

image
na SAMUEL MAINA

Burudani08 December 2023 - 12:24

Muhtasari


  • •Antoneosoul alikuwa miongoni mwa mastaa walikuwepo wakati chama cha UDA kilipozindua harakati za toroli mnamo 2021.
  • •Video za Anto Neosoul na watu wengine mashuhuri wakimsukuma Ruto alipokuwa ameketi kwenye toroli zinavuma mtandaoni.
akitoa huduma ya MC wakati wa uzinduzi wa UDA.

Mwanahabari Anto Neosoul amekiri kuwa hakulipwa kwa kazi ya MC aliyopewa kufanya wakati wa hafla ya uzinduzi wa chama cha Rais Ruto mwaka wa 2021.

Video za Anto Neosoul na watu wengine mashuhuri wakimsukuma Ruto alipokuwa ameketi kwenye toroli zinavuma mtandaoni.

Mkenya kwenye mtandao wa X.com ConradKulo alitumia video hiyo kuzungumzia vijana

"Katika kipindi kilichopita cha Mboka na William Ruto, vijana waomoke." Mwanamtandao huyo alicheka huku mwingine akimtaja Anto Neosoul kwa GIF na kumfanya mwanahabari huyo kukiri kuwa hakulipwa.

"Na unajua mimi sichezi na pesa zangu! Lakini wueeeeh," Anto aliandika

Hapa kuna maoni zaidi kutoka kwa Anto Neosoul na mashabiki

@Maw1ra....Hiyo kubebwa ndio ilikua pay yako ni kama130...@antoneosoul•...A literal FREE RIDE!

@AyTanzania....Hukuapply ile trick ya Lagos?2208.7KAnto Neosoul @antoneosoul•....Hehehe umenifunza kutoruhusu watu wacheze na pesa zangu…. I’ll never forget that… but nilipatana na Pwaguzi!

@irenenjokikar..... Ati hukulipwa? @antoneosoul•...Wallai

@AlhajiKe....Unasema pastor alikutumia kuvuka mto jordan @antoneosoul•...Niliachwa kwa meli Kati Kati ya mto Jordan. Macho.

Jina la chama cha UDA na alama ya toroli ilikuwa sahihi ya Ruto wakati wa kampeni.

UDA baada ya kujiandikisha ilianza kampeni kali ya kujibadilisha ikiwa ni pamoja na kupata ofisi pana katika Barabara ya Makindi ya Kilimani iitwayo Hustler's Centre.

Ruto alikuwa akifanya kampeni katika kinyang'anyiro cha Urais 2022 na kutoa changamoto kwa vijana kujitokeza na kuhesabiwa katika uchaguzi mkuu akiongeza kuwa wanaunda idadi kubwa zaidi ya wapiga kura.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved