logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Pritty Vishy amdhihaki Stevo kufuatia madai ya mkewe kupachikwa mimba na jamaa mwingine

Pritty Vishy alidokeza kwamba tayari alikuwa akijua kuhusu drama ambazo zimegonga ndoa ya mpenzi wake wa zamani.

image
na SAMUEL MAINA

Burudani19 December 2023 - 09:23

Muhtasari


  • •Pritty Vishy alidokeza kwamba tayari alikuwa akijua kuhusu drama ambazo zimegonga ndoa ya mpenzi wake wa zamani.
  • •Vishy alidai kuwa Stevo alimcheza na Grace Atieno ambaye sasa inasemekana alim’cheat na hata kupata ujauzito wa mwanaume mwingine.
Stivo Simple Boy na aliyekuwa mpenzi wake Pritty Vishy

Mtayarishaji maudhui, Purity Vishenwa, kwa jina maarufu Pritty Vishy, amemdhihaki mpenzi wake wa zamani Stevo Simple Boy huku kukiwa na uvumi wa matatizo katika ndoa yake.

Kumekuwa na tetesi nyingi kwenye mitandao ya kijamii zikidai kuwa Stevo na mke wake Grace Atieno hawako katika maelewano mazuri tena baada ya mwimbaji huyo kudaiwa kubaini kuwa mpenzi huyo wa maisha yake alikuwa amepachikwa mimba na mwanaume mwingine.

Wakati akijibu uvumi huo, Pritty Vishy alidokeza kwamba tayari alikuwa akijua kuhusu drama ambazo zimegonga ndoa ya mpenzi wake wa zamani.

"Shawrry wa uchungu alijua buana, sio kwamba ninafuata maisha ya ex wangu lakini kwa sababu yuko karibu na rafiki yangu. Yooh, mambo ni mabaya zaidi si vile mnadhani,” Pritty Vishy alisema kupitia akaunti yake ya Instagram Jumanne asubuhi.

Aliongeza zaidi “Kutoka kwa “Pritty alikuwa ananicheat na wanaume 50” kwenda “maex wakae kando” alafu… “mimba sio yangu alinicheat”.. eei, hamuoni budesko ako na ngori, mara management, mara tudem amedate wote wamecheat.”

Mrembo huyo mwenye umri wa miaka 22 aliendelea kudai kuwa Stevo Simple Boy alimcheza na mkewe wa sasa Grace Atieno ambaye sasa inasemekana alim’cheat na hata kupata ujauzito wa mwanaume mwingine.

Vishy alidai kuwa mke wa Stevo alimfuata msanii huyo wa Kibera kwa nia ya pesa lakini baadaye akagundua kuwa mambo hayakuwa sawa kama alivyofikiria.

"Kwa hiyo msichana alijisikia vizuri sana wakati mtu X alikuwa akinicheza na yeye .. alifikiri mtu huyo X alikuwa na mula mwingi, hivyo nilipoondoka alifurahi na kuamua kuhama naye ili kujua tu .... mmmh, akadhani menejimenti ilikuwa mbovu sana ambayo ni kweli kwani “mtu wake” omusanii hajui kujisimamia kama mwanaume.. Mzuri mitandaoni.. akaamua kuishusha menejimenti ambayo ilikuwa sawa lakini hakuwa nayo. plan B kama vile nilivyokuwa, kwa hivyo ikabaki omusanii ako penye ako,” Pritty Vishy alisema.

Mtayarishaji maudhui huyo aliendelea kumshutumu mke kwa Stevo kwa kum’cheat mwanamuziki huyo na mwanaume mwingine kwani hakuweza kupata pesa na kuridhika anakohitaji.

Aidha, alidai kuwa Stevo aligundua kuwa ujauzito wa mkewe sio wake baada ya kufanya hesabu zake vizuri.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved