logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Aliyekamata mkewe aki'cheat na jamaa mwingine achapisha picha zao kwenye Tshirt yake

Alimtembelea mkewe kazini akiwa ameivaa tsheti hiyo.

image
na Davis Ojiambo

Burudani03 January 2024 - 13:49

Muhtasari


  • • Alisababisha mijadala kuhusu mahusiano, ukafiri, na jinsi watu wanavyokabiliana na maumivu ya kihisia kwa njia tofauti.

Katika miaka ya hivi karibuni, ulaghai wa mapenzi haswa katika ndoa pamoja na usaliti limekuwa jambo la kawaida sana ambalo linatekelezwa na wanaume na wanawake.

Wakati huo huo pia kumekuwa na fumanizi nyingi ambazo hupelekea matokeo ambayo si ya kufurahisha, ikiwemo mauaji kutokana na hasira lakini pia mtu kujiua baada ya kuhisi moyo wake kuchezewa shere.

Lakini janaa mmoja ameibuka na mbinu mpya kabisa ya kulipa kisasi baada ya kumfumani mke wake akichepuka na mwanamume mwingine.

Katika picha za mwanamume huyo ambazo zilishirikiwa kwenye mtandao wa X na mtumizi mmoja kwa jina @PeopleWithIQ, mwanamume huyo baada ya kuwafumani, hakuwadhuru kwa njia yoyote kimwili, bali aliamua kuwadhuru kisaikolojia Zaidi, kivipi?

Mwanamume huyo alipomfumania mkewe akishiriki mapenzi na mwanamume mwingine, alichukua picha zao na kuondoka nazo kisha akazichapisha kwenye upande wa mbele wa Tsheti yake.

Mwanamume huyo wala hakuishia hapo, baada ya kuchapisha picha hizo kwenye Tsheti, aliamua kufanya ziara ya kumtembelea mkewe katika ofisi ambako alikuwa anafanya kazi, akiwa ameivaa Tsheti hiyo.

Picha za T-shirt zimeenea kwenye mitandao ya kijamii, na kusababisha mijadala kuhusu mahusiano, ukafiri, na jinsi watu wanavyokabiliana na maumivu ya kihisia kwa njia tofauti.

Chapisho hilo linasema, “Mwanaume huyu alimshika mkewe akichepuka. Akawapiga picha, akaiweka kwenye fulana na kwenda kumuona kazini akiwa amevaa shati hilo”.

Chapisho hilo limevutia hisia mseto, baadhi wakimkosoa kwa kuamua kumdhalilisha mkewe hadharani hadi maeneo yake ya kazini.

Lakini wengine pia walimsifia kwa kutochukua maamuzi magumu ya kumuumiza au kuwajeruhi alipowafumani, na badala yake kuchukua msimamo tofauti kabisa wa kuwafanya wahisi uchungu pasi na kuwadhuru kimwili.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved