logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Wanaume zaidi ya 200 watuma maombi ya kuchangia mbegu za kiume kwa malipo!

Alisema ugumu wa kiuchumi umewafanya watu wote kuhangaika vibaya na kujitoa kwa lolote.

image
na Davis Ojiambo

Burudani05 February 2024 - 07:31

Muhtasari


  • • "Kujitolea lazima kuwa AA na bila magonjwa. Malipo ni 900k. Chukulia haraka, unaweza hata kutoa mitungi miwili.” chapisho lilisoma.
Mwanamume afikishwa mahakamani kuzuiwa kuchangia mbegu za kiume zaidi baada ya kuzalisha watoto zaidi ya 550.

Mwanamume mmoja katika mtandao wa kijamii ameonyesha kushtushwa kwake na idadi ya wanaume ambao wametuma maombi ya kuchangia mbegu zao za kiume kwa ajili ya kupata pesa.

Ilinza pale ambapo jamaa huyo kwa jina Ukan Kurugh aliweka tangazo kwamba angetaka wanaume wajitolee kuchangia mbegu za kiume kwa ajili ya malipo, akiliweka tangazo hilo kuwa wito wa haraka kwa yeyote mwenye uwezo wa kuchangia.

Tangazo hilo lake la Februari mosi lilisema kwamba kila atakayejitolea kuchangia mbegu zake za kiume atapata Zaidi ya laki 9 taslimu, lakini kwa mshangao wake, Zaidi ya wanaume 200 walifurika katika Inbox yake wakisema wako tayari kufanya hivyo.

Chapisho hilo linasema, “Mchangiaji wa manii anahitajika Abuja. Kujitolea lazima kuwa AA na bila magonjwa. Malipo ni 900k. Chukulia haraka, unaweza hata kutoa mitungi miwili.”

Kulingana na Ukah, amepokea jumbe za wanaume zaidi ya 200 wakionyesha nia yao ya kutoa mbegu za kiume.

Ukan Kurugh, anayejitambulisha katika mtandao huo kama mwanaharakati wa kibinadamu, alielezea mshangao wake na wasiwasi wake katika chapisho siku ya Ijumaa, akionyesha matatizo ya kiuchumi ambayo watu nchini humo wanakabili.

Aliona kuwa mwitikio mkubwa kwa ombi la mchango wa manii unaonyesha jinsi Wanaume walivyo tayari kwenda kwa utulivu wa kifedha katika uchumi mgumu.

Msaidizi huyo wa kibinadamu pia alitambua hali mbaya ya watu wanaouza mali ili kupata riziki.

Aliandika, "Ni dhahiri kuwa watu wanateseka katika nchi hii na watafanya chochote kupata pesa," aliandika kwenye chapisho mnamo Ijumaa.

"Chapisho nililotoa kuhusu utoaji wa mbegu za kiume limemaliza kikasha changu na watu zaidi ya 210 wakisubiri anwani/mahali. Wanawake wanapotoa mayai, ni wanaume ambao huwa wagumu kwao lakini wanaume wanachukua nafasi polepole.

"Ukweli wa kusikitisha ni kwamba watu wanaweza kuuza chochote kinachowezekana ili maisha yaendelee kuwaendea. Kwa kweli inasikitisha na tunaweza tu kuwa na matumaini mazuri na hali ya kusikitisha ya uchumi hivi sasa.”

Tazama chapisho hilo hapa;


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved