Kate Actress ajivinjari na mpenziwe mpya jijini Dubai, washiriki nyakati za kimapenzi (+video)

Muigizaji huyo alichapisha video zake na Bw Mwangi wakiburudika na kujivinjari katika maeneo tofauti.

Muhtasari

•Kate yuko pamoja na mpenzi wake wa sasa Michael Mwangi, ambaye amekuwa akiburudika naye katika nchi hiyo ya Mashariki ya Kati.

•Muigizaji huyo na mpenzi wake walionekana wakipanda gari pamoja kabla ya kuonekana kwenye sehemu ya burudani.

na mpenziwe mpya.
Kate Actress na mpenziwe mpya.
Image: HISANI

Muigizaji wa Kenya aliyeshinda tuzo nyingi, Catherine Kamau almaarufu Kate Actress anaendelea kufurahia muda jijini Dubai ambako anasherehekea siku yake ya kuzaliwa.

Kate, ambaye aliadhimisha siku yake ya kuzaliwa ya 37 mnamo Februari 3 yuko pamoja na mpenzi wake wa sasa Michael Mwangi, ambaye amekuwa akiburudika naye katika nchi hiyo ya Mashariki ya Kati.

Siku ya Ijumaa, mama huyo wa watoto wawili alishiriki video zake na Bw Mwangi wakiburudika na kujivinjari katika maeneo tofauti.

Katika moja ya video hizo, wapenzi hao wawili walionekana kwenye hoteli moja ya kifahari ambapo waliketi kwenye meza iliyojaa vitu tofauti vya kunywa na kula. Juu ya meza, pia kulikuwa na barua zenye jumbe za kheri ya siku ya kuzaliwa.

"Heri ya siku ya kuzaliwa Catherine. Nakutakia wakati mwema katika siku yako,” moja ya maelezo hayo yalisomeka.

Katika video nyingine, muigizaji huyo na mpenzi wake walionekana wakipanda gari pamoja kabla ya kuonekana kwenye sehemu ya burudani ambapo waliburudika na marafiki wengine.

Uhusiano mpya wa Muigizaji Kate Actress ulikuja kujulikana mwishoni mwa mwaka jana baada ya mama huyo wa watoto wawili kuanza kuonekana hadharani na mpenzi huyo wake mwenye ndevu nyingi. Haijabainika wawili hao wamekuwa wakichumbiana kwa muda gani lakini sasa ni wazi kuwa ni wapenzi.

Kabla ya uhusiano wake wa sasa, mama huyo wa watoto wawili alikuwa ameolewa na muigizaji mwenzake, Phillip Karanja kwa takriban miaka sita.

Kate Actress amethibitisha kwamba ni kweli yeye na mpenzi wake ambaye ni muongozaji wa video, Phil Karanja si wapenzi tena.

Muigizaji huyo aliweka haya wazi kupitia instastori zake ambapo alipakia ujumbe wa kusema kwamba ni kweli waliachana muda mrefu uliopita ila waliafikiana kuliweka suala hilo kinyemela ili kushughulikia masuala Fulani.

Alipakia ujumbe huo uliokuwa na maandishi kwamba ni kutoka kwa pande zote, yeye na Phil na kuwataka mashabiki wao kukubaliana na uamuzi wao kwamba mambo yalishindwa kutengemaa.

“Tulifikia uamuzi wa kuvunja ndoa yetu muda mrefu uliopita na tukatengana. Kwa kweli tunaomba kila mtu kuheshima uamuzi wetu kwa ajili ya maisha yetu ya faraghani lakini pia na ya watoto wetu,” ujumbe huo mfupi ulisoma.