Betty Kyallo azungumzia kumzalia mpenzi wake mpya

Katika majibu yake, Charlie alimwomba mama wa binti mmoja wazae naye watoto zaidi.

Muhtasari

•Betty alikuwa amechapisha ujumbe akikiri mapenzi yake mengi kwa kijana huyo wa miaka 26 wakati mazungumzo yao ya kusisimua yalipoanza.

•Katika ujumbe wake kwa mpenzi wake usiku wa kuamkia Ijumaa wiki iliyopita, Betty Kyallo alimtakia mambo mema na kwa uhusiano wao.

amemtambulisha mpenziwe mpya.
Betty Kyallo amemtambulisha mpenziwe mpya.
Image: INSTAGRAM// BETTY KYALLO

Mwanahabari Betty Kyallo alijibu la kizushi baada ya mpenzi wake Charlie Jones kuomba kuzaa naye.

Mtangazaji huyo wa TV alikuwa amechapisha ujumbe akikiri mapenzi yake mengi kwa kijana huyo wa miaka 26 wakati mazungumzo yao ya kusisimua yalipoanza.

"Habari mpenzi! Nakupenda wewe!” Betty alimwandikia mpenzi wake.

Katika majibu yake, Charlie alimwomba mama wa binti mmoja wazae naye watoto zaidi.

"Nipe watoto," Charlie aliandika.

Betty akajibu, “Oh neno? Sema kidogo."

Haya yanajiri siku chache tu baada ya wapenzi hao wawili kuweka wazi uhusiano wao huku Betty akikiri kumpenda kijana huyo wakati akisherehekea siku yake ya kuzaliwa ya 26.

Katika ujumbe wake kwa mpenzi wake usiku wa kuamkia Ijumaa wiki iliyopita, Betty Kyallo alimtakia mambo mema na kwa uhusiano wao.

"Heri ya kuzaliwa mpenzi. Vicheko zaidi, furaha zaidi, kukumbatiana zaidi, watoto zaidi, sisi zaidi. Ni hivi,” Betty Kyallo aliandika kwenye mtandao wa Instagram.

Aliambatanisha ujumbe wake na picha nzuri yake na mwanaume huyo. Pichani, mwanamume huyo anaonekana kuwa mrefu zaidi na ana rasta kichwani.

Mama huyo wa binti mmoja aliendelea kumshukuru mpenzi wake na kusherehekea mapenzi yao.

"Asante kwa kila kitu. Heri ya kuzaliwa,” aliandika.

Kyallo alijigamba kwa kujipatia mwanamume anayefaa na kuwapuuza kila mtu mwingine.

“Mungu alinitumia aliye sahihi. Nyinyi nyote mnaweza kuwa na hasira,” alisema.

Pia alijigamba kuhusu kuwa na furaha na mpenzi wake mpya na kumtakia mwanaume huyo mafanikio zaidi.

"Naomba mtu wangu ashinde kila wakati. Anashinda lakini nataka ashinde mengi zaidi. Juu ya Mungu. Furaha mke, maisha ya furaha,” alisema.