Kanyari adai katibu wake ndiye alitoa wazo la sadaka ya 310

" Nisingefurahia maisha niliyo nayo sasa kama si mwanamke huyo.” Kanyari alisema.

Muhtasari

•Akiwahutubia waumini wa kanisa lake, Kanyari alisimulia majaribio yao yasiyofaulu ya kuomba matoleo ya KSh 500 na KSh 1,000.

•Alimsifu katibu huyo kwa kuleta mawazo ya kibunifu kwenye meza yake na kuwashauri wafuasi wake kuunga mkono wale wanaowaunga mkono.

Pastor Kanyari
Pastor Kanyari
Image: HISANI

Mhubiri mashuhuri wa Kenya Victor Kanyari ameeleza kuwa katibu wake ndiye aliyetoa wazo la sadaka ya KSh 310 lakini sio yeye kama wengi husema.

Akiwahutubia waumini wa kanisa lake, Kanyari alieleza kwa kina jinsi walivyojaribu pesa mbalimbali, kama vile KSh 500, KSh 1000, na KSh 700, lakini hakuna iliyofaulu.

 Ni hadi walipoomba KSh 310 ndipo walipopokea zaidi ya shilingi milioni 1 kwa siku moja, hali iliyopelekea katibu huyo kumshauri kushikilia kiasi hicho cha pesa.

"Nilikuwa na mwanamke mmoja hapa ambaye alienda Amerika, alikuwa katibu wangu.

Ndiye aliyetoa wazo la 310. Sio mimi kama wengine husema. Tuliomba KSh 1000 lakini hakuna aliyetuma.

Tuliomba pia KSh 700 lakini hakuna aliyetuma siku tulipoomba KSh 310, tulipata milioni moja na mwanamke huyo akaniambia katalia hapo.

 Nisingefurahia maisha niliyo nayo sasa kama si mwanamke huyo.” Kanyari alisema.

 Kanyari pia aliongeza kuwa mwanamke huyo anapompigia simu bado huwa anachagua kumsikiliza.

Pia alisisitiza umuhimu wa kuthamini wale wanaotoa mwongozo na msaada.