Kutana na mrembo ameishi na ubikira kwa miaka 33 kwa kuwa na masharti 12 kwa wanaume

Anaangazia mwanamume kuwa; mkweli, Mrefu kuliko yeye, mwenye mwili wa kiriadha-riadha hivi, anayependa kusafiri, mwenye hajawahi kuoa awali, mwenye uthubutu, mcheshi, mtulivu, na wa kumheshimu yeye.

Muhtasari

• Noble yuko sana kwenye mitandao ya kijamii, ambapo anashiriki shughuli zake za kila siku. Ingawa anataka uhusiano, anachagua sana.

• "Nina viwango vya juu na sidanganyi," alisema katika mahojiano, iliyoripotiwa na New York Post.

 
• Noble alikiri kuwa hajawahi kuwa kwenye uhusiano mzito. Uhusiano wake mrefu zaidi ulidumu siku tatu tu. Licha ya hayo, yeye haachi tumaini la kupata mwenzi kamili.

DONYELLE NOBLE
DONYELLE NOBLE
Image: Facebook

Mrembo mmoja mwenye umri wa miaka 33 amedai kuwa masharti yake magumu kwa wanaume wanaojaribu kumtongoza yamesababisha yeye kuwa bikira hadi sasa.

Kwa mujibu wa jarida la The New York Post, Danyele Noble kutoka jimbo la Florida anaorodhesha vigezo 12 ambavyo mwanaume lazima afikie kabla ya kuamua kuwa na uhusiano naye.

Kutokana na hilo, wanaume wengi ambao wanashindwa ku’tick maboksi yote 12 wameishia kumtenga na mpaka kufikia umri wa miaka 33, bado hajawai kushiriki tendo la ndoa ila anatumai mwanamume wake yupo njiani.

Noble yuko sana kwenye mitandao ya kijamii, ambapo anashiriki shughuli zake za kila siku. Ingawa anataka uhusiano, anachagua sana.

"Nina viwango vya juu na sidanganyi," alisema katika mahojiano, iliyoripotiwa na New York Post.

Noble alikiri kuwa hajawahi kuwa kwenye uhusiano mzito. Uhusiano wake mrefu zaidi ulidumu siku tatu tu. Licha ya hayo, yeye haachi tumaini la kupata mwenzi kamili.

"Nilikuwa nikiona aibu kuwaambia watu kuhusu hilo. Ningependa kusema uwongo tu na kusema, 'Hapana, mimi si bikira,' lakini kuzungumza juu yake mara kwa mara kumenifanya nitambue kwamba hakuna ubaya na hilo. Watu wengi wanaheshimu hilo."

Mahitaji yake yanahusu sifa zote mbili za utu na mwonekano wa mwenzi anayewezekana.

Kwa mujibu wa jarida hilo, Noble anaangazia mwanamume kuwa; mkweli, Mwenye moyo mwema, Mrefu kuliko yeye, mwenye mwili wa kiriadha-riadha hivi, anayependa kusafiri, anayependa maisha ya nje ya nyumba, mwenye hajawahi kuoa awali, mwenye uthubutu, mcheshi, mtulivu, na wa kumheshimu yeye.