Mwanamke adai yeye ndiye ‘Bikira Maria Mtakatifu’ mama wa Yesu (video)

"Mungu alinifunulia kujua kwamba mimi ndiye mama wa Yesu. Na huu ufunuo umekuwa ukinijia tangu 2015, nimekuwa nikipata maono mengi na Yesu alizaliwa kupitia mimi.”

Muhtasari

• Katika video hiyo, mwanamke huyo anasikika akizungumza kuhusu kuwa na maono wakati akitangaza kuja kwa Yesu duniani.

Anayedai kuwa Maria mama wa Yesu
Anayedai kuwa Maria mama wa Yesu

Mwanamke mmoja kutoka nchini Nigeria anayedai kuwa yeye ni Mariamu mtakatifu amezua mjadala akidai Yesu anatoka Nigeria.

Hii ilifichuliwa katika chapisho jipya lililozua mawimbi kwenye jukwaa maarufu la mitandao ya kijamii.

Katika video hiyo, mwanamke huyo anasikika akizungumza kuhusu kuwa na maono wakati akitangaza kuja kwa Yesu duniani.

 

Anasikika akifichua kuwa yeye ni Bikira Maria kama ilivyofunuliwa kwake, huku akitangaza kwa ujasiri kwamba Yesu ni Mnigeria kutoka Jimbo la Imo, haswa kutoka eneo la serikali ya mtaa liitwalo Mbaitoli.

 

Alishikilia kuwa yeye ni mama yake Yesu na Maria Mtakatifu kwenye video hiyo, ambayo imevutia maelfu ya watu waliotazamwa mtandaoni.

Kwa maneno yake;

“Ndio, Yesu anatokea Nigeria. Mimi ndiye mama wa Yesu na yeye usuli wake ni Nigeria. Mungu alinifunulia kujua kwamba mimi ndiye mama wa Yesu. Na huu ufunuo umekuwa ukinijia tangu 2015, nimekuwa nikipata maono mengi na Yesu alizaliwa kupitia mimi.”

“Kwa mujibu wa maono ambayo ninapata, mimi ndiye Bikira Maria mtakatifu mama wa Yesu na Yesu atakuja tena kupitia mimi katika ujio wake wa pili duniani, na hicho ndicho ambacho Mungu ameniagiza kutangaza.”

Tazama video hiyo hapa chini kisha utoe maoni yako.