Mke amshtaki mumewe kwa pasta baada ya kuuza pikipiki 3 za mamake kucheza kamari

Katika video hiyo ambayo sasa inavutia maoni kinzani katika mtandao wa TikTok, mrembo huyo alimpeleka mumewe kwa pasta na kumshtaki kwamba uraibu wake kwa Kamari umevuka viwango.

Muhtasari

• Alifichua kuwa mamake mumewe, ambaye ni mfanyabiashara, amekuwa akiwasaidia kifedha.

•  Aliomboleza kwa uchungu mchungaji aje kuwaokoa kwa kumtoa mume.

 

Mwanamke mmoja amezua gumzo katika mitandao ya kijamii baada ya kumburuza mumewe kwa nguvu moja kwa moja hadi kwa mchungaji wa kanisa analoshiriki na kumshtaki kwa pasta kwa kuwa na uraibu wa Kamari.

Katika video hiyo ambayo sasa inavutia maoni kinzani katika mtandao wa TikTok, mrembo huyo alimpeleka mumewe kwa pasta na kumshtaki kwamba uraibu wake kwa Kamari umevuka viwango kiasi kwamba amevikia hatua ya kuuza vitu na mali ya boma ili kucheza Kamari.

Alisema kwamba mumewe amefikia hatua mpaka ya kuuza bodaboda za mama yake na kupeleka hela zote kucheza mchezo wa bahati nasbu, na mwisho wa siku kuishiwa kupoteza hela zote na kurudi nyumbani mikono mitupu akilenga kuuza kitu kingine tena kwa nia ya kwenda kuzikomboa hela alizopoteza awali.

Alifichua kuwa mamake mumewe, ambaye ni mfanyabiashara, amekuwa akiwasaidia kifedha. Aliomboleza kwa uchungu mchungaji aje kuwaokoa kwa kumtoa mume.