Mrembo amtaka Ex kumfidia kwa kumharibia muda na kumuacha bila kumuoa kisa ni maskini

Mrembo huyo alisema kuwa mpenzi wake alikatisha uhusiano wao ghafla akitumia kisingizio kwamba alitaka kuwa pasta na baba yake alikuwa amemshauri kutooa mwanamke kutoka familia maskini.

Muhtasari

• Kisa hicho, kilichonaswa kwenye video inayosambazwa kwenye TikTok kupitia @oheneniadazoaofficial, kimeibua hisia nyingi mtandaoni.

Mwanamke mmoja raia wa Ghana ametumia mitandao ya kijamii kuonyesha mafadhaiko yake kwa aliyekuwa mpenzi wake kwa kumuacha baada ya kukaa katika uhusiano kwa muda mrefu.

Kwa mujibu wa mrembo huyo ambaye alionekana Dhahiri kuumia kutoka ndani ya moyo wake, alisema kwamba mpenzi wake alikatisha uhusiano wao ghafla akisema hatamuoa kwa vile yeye ni maskini na si type yake.

Mrembo huyo sasa alitaka kusaidiwa njia salama ya kisheria ili kupata haki yake ya fidia, akisema kuwa mwanamume huyo alimuaharibia muda wake kwa ahadi kwamba angemuoa na mwisho wa siku akamtelekeza kwenye mataa asijue pa kuanzia.

Kisa hicho, kilichonaswa kwenye video inayosambazwa kwenye TikTok kupitia @oheneniadazoaofficial, kimeibua hisia nyingi mtandaoni.

Katika video hiyo, ambayo ilionekana kwenye Sompa Nkomo kwenye runinga ya Sompa, mwanamke huyo alilalamikia uamuzi wa ghafla wa mpenzi wake kusitisha uhusiano wao.

Mrembo huyo alisema kuwa mpenzi wake alikatisha uhusiano wao ghafla akitumia kisingizio kwamba alitaka kuwa pasta na baba yake alikuwa amemshauri kutooa mwanamke kutoka familia maskini.

"Aliniahidi angenipeleka nje ya nchi, na ninataka atimize ahadi hiyo," alisema kwa sehemu.