logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Jamaa azawadiwa Ksh 643k baada ya kurudisha Ksh 1.8M zilizotumwa kwake kimakosa

DAYYWALKER98 alisema: "Mungu alikujaribu na ukafaulu!!"

image
na Davis Ojiambo

Burudani03 July 2024 - 11:14

Muhtasari


  • • Akishiriki furaha yake kwenye Twitter, Femi aliandika; "Waoh $5000 hii inashangaza. Ahsante Mungu kwa kuniwezesha kuchukua maamuzi yaliyo sahihi."
Jamaa aliyetunukiwa kwa uwazi wake

Ukisikia kulala maskini na kuamka tajiri basi ndio hii.

Mwanaume mmoja amehadithia jinsi maisha yake yalibadilika ghafla baada ya kuonyesha kitendo cha kutokuwa na pupa.

Mwanamume huyo alisema alitumiwa kiasi kirefu cha pesa, doll elfu 14 za Marekani sawa na shilingi milioni 1.8 za Kenya katika simu yake kutoka kwa mtu asiyemjua.

Baadae mtu yule alimpigia simu akimuomba aweze kuzirudisha kwani alikosea namba.

Bila kusita, Jamaa huyo alisema alirudisha pesa hizo ba asichokijua ni kwamba yule mtu alikuwa muungwana na baada ya dakika kidogo alimtumia doll elfu 5, sawa na laki 6 na elfu 43 pesa za Kenya.

Akishiriki furaha yake kwenye Twitter, Femi aliandika; "Waoh $5000 hii inashangaza. Ahsante Mungu kwa kuniwezesha kuchukua maamuzi yaliyo sahihi. @raffayalvi,"

Wanamitandao walimhongera kwa ukarimu wake, wengine wakisema ni kama majaribu kutoka kwa Mungu ambapo alifuzu mtihani wake.

Maoni ya Wanamtandao...

@Kents29 alisema: “Bro ondoa kwanza kabla hujafanya biashara ya o. "Kujiondoa ndio njia pekee ya kushinda. "Pls ondoa kwenye akaunti yako kwanza."

@Adebayo_Dex alisema: “Watu ambao hawakukumbuka kabla hawajaanza kukupigia simu? "Hapana chukua simu zao oooo."

@orseaboh alisema: "Nadhani unahitaji kuthamini jumuiya unayoikuza pia."

@DAYYWALKER98 alisema: "Mungu alikujaribu na ukafaulu!!"


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved