Mfanyibiashara alia hasara baada ya tuktuk iliyombebea mayai kuanguka na kuyavunja yote (video)

Kwa bahati mbaya, tuktuk ile ilihusika katika ajali kidogo na kuanguka kwa kupinduka, jambo lililopelekea kreti zote za mayai kuanguka na mayai karibia yote kuvunjika na kutapakaa kwenye barabara.

Watumizi wa mitandao ya kijamii wamemhurumia mfanyibiashara mmoja baada ya mtaji wake kuharibika katika ajali.

Video hiyo kwenye mtandao wa TikTok ilinasa tukio hilo la kutia huruma ambapo mfanyibiashara huyo wa kuuza mayai alikuwa akiyasafirisha kwenda sokoni kwa kutumia usafiri wa tuktuk.

Kwa bahati mbaya, tuktuk ile ilihusika katika ajali kidogo na kuanguka kwa kupinduka, jambo lililopelekea kreti zote za mayai kuanguka na mayai karibia yote kuvunjika na kutapakaa kwenye barabara.

Video hiyo ilichapishwa kwenye mtandao wa kijamii, TikTok na mwanamtandao anayejulikana kama @franknailsandmakeup.

Jinsi ajali hiyo ilivyotokea haijajulikana, hata hivyo, tuktuk ya kubebea mizigo ilionekana kupinduka huku kreti nyingi za mayai iliyokuwa imebeba zikiwa zimezagaa chini, zimevunjwa.

Pikipiki iliyokuwa imegongana nayo pia ilionekana ikiwa imelala chini katikati ya maganda ya mayai yaliyovunjika.

Watu walikusanyika pande zote kushuhudia fujo kwani wengine walisikika wakieleza huruma zao juu ya msiba mkubwa.

Abu Audrey alisema: "hiyo ni takriban 600 hadi 700k 😭😭😭"

mtumiaji4220162661781 akajibu: “hapana kaka, ni zangu! zina thamani ya 10M😢😢😢”

mummyT 4 real🤣 alisema: "inasikitisha sana!! mbona uzembe hivi!!! chaiii suluhu itakuwa nini sasa?🙏”

Sucre_24 aliandika: "Itakuwaje ikiwa ni mkakati wa kutupa mayai mabaya kwa gharama?"

swabulahbntmhd24 alisema: "lakini unawezaje kuweka mayai yote kwenye aboda boda"

@missy aliandika: “Wakati kijijini kwako watu wanakufuata na kukuahidi kutokuacha uende😂😂😂”