logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Miaka 500 ijayo uso wangu utatumika kumwakilisha Yesu Kristo, pasta adai (video)

“Picha zangu zitachukua nafasi ya Kristo katika miaka 500 ijayo.”

image
na Davis Ojiambo

Burudani09 July 2024 - 13:19

Muhtasari


  • • Katika video hiyo, Mchungaji Kyei-Duah anatangaza kwa ujasiri kwa waumini wake kwamba picha zake zitachukua nafasi ya zile za Yesu Kristo katika kipindi cha karne tano zijazo.

Mchungaji mmoja amezua minong’ono mingi katika mtandao wa kijamii baada ya kuonekana akiwahubiria waumini katika kanisa lake akitabiri kwamba atakuwa kama Yesu katika kipindi cha miaka 500 ijayo.

Video hiyo yenye utata ya mchungaji wa Ghana aliyetambulika kwa jina Stephen Adom Kyei-Duah, alionekana bila hiana akidai kwamba atachukua nafasi ya Yesu Kristo katika maisha ya wanadamu katika miaka 500 ijayo.

Katika mahubiri hayo, mchungaji huyo alionekana akiwaambia waumini wake kwa sauti ya kutisha kwamba picha zake zitakuwa zinasambazwa kwa Wakristu kote duniani na wataziweka kwenye kuta za nyumba zao wakimuangalia na kumtafsiri kama Yesu.

Katika video hiyo, Mchungaji Kyei-Duah anatangaza kwa ujasiri kwa waumini wake kwamba picha zake zitachukua nafasi ya zile za Yesu Kristo katika kipindi cha karne tano zijazo.

Mchungaji Kyei-Duah alitangaza wakati wa mahubiri, “Picha zangu zitachukua nafasi ya Kristo katika miaka 500 ijayo.”

Kauli ya mchungaji huyo imezua dhoruba ya ukosoaji na kutoamini mtandaoni, huku watumiaji wengi wakionyesha kushtushwa na kutokubali madai hayo ya kufuru.

Tazama video hiyo hapa kisha utoe maoni;


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved