Mrembo auza ndugu yake kwa Ksh 34k, ampa mchumba pesa kununua vitu vya harusi yao

Binti huyo wa miaka 24 alimdanganya mama yake na kumtaka kumruhusu kuondoka na ndugu yake wa miaka 3 kijijini kwa lengo la kumweka katika shule nzuri mjini, kabla ya kumpiga mnada ili kupata pesa za kupanga harusi.

Muhtasari

• Mwanamke huyo alilaumu hali ngumu ya kiuchumi nchini humo kama sababu ya hatua yake ya kukata tamaa.

Mwanamke aliyefungwa jela pingu mikononi.
Mwanamke aliyefungwa jela pingu mikononi.
Image: Shutterstock

Mwanamke mwenye umri wa miaka 24, amekiri kumuuza ndugu yake wa miaka mitatu (jina linahifadhiwa) kwa gharama ya naira 410,000] sawa na Ksh 34k] ili kupata pesa za harusi yake ya jadi na mahitaji mengine.

Mwanamke huyo mkazi wa Mubi katika Jimbo la Adamawa nchini Nigeria, huku ndugu yake akiishi na mama yao mbali na anakoishi yeye.

Inasemekana kwamba mshukiwa alimhadaa mamake kabla ya kumchukua mtoto huyo kwa kisingizio cha uwongo cha kumwandikisha katika shule ya Mubi, kilomita 40 hivi kutoka Rimirgo alikokuwa akiishi na mama yake.

Baada ya wiki kadhaa, mama yao aliingiwa na wasiwasi kwani majaribio yake yote ya kuzungumza na mwanawe kupitia simu yalizuiwa kwa ujanja na bintiye.

Mama aliamua kueleza hali hiyo kwa polisi, hali iliyosababisha kukamatwa kwa mtuhumiwa.

Akisimulia tukio hilo, binti huyo alisema alimuuza mvulana huyo kwa naira 410,000 kwa mnunuzi aliyekuwa tayari, ambaye alisafirisha mwathiriwa huyo hadi mji wa Enugu katika jimbo la kusini mashariki la Enugu.

"Nilitumia mapato ya uhalifu huo kununua mashine ya kusaga ili nianze biashara na pia nilimpa mpenzi wangu ₦ 200,000 kununua vitu vinavyohitajika kwa ajili ya harusi yetu ya kitamaduni," mshukiwa alikiri mbele ya polisi kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo.

Kwa upande wake, mama alionyesha kusikitishwa, akishangaa jinsi binti yake angeweza kumuuza ndugu yake kwa mtu asiyemjua kabisa.

"Alinitembelea mwaka jana na kunidanganya kwamba angemchukua kaka yake wa kiume ili kumuandikisha katika shule moja mjini, kwa kuwa hakuna shule nzuri kijijini kwetu.”

"Tangu alipomchukua yule kijana sikuwahi kumsikia kwani muda wowote nilipopiga simu ili kusikia sauti yake alikua akiniambia uwongo mmoja au mwingine kwa muda wa mwaka mmoja sasa. Nilichoka kuuliza na kwa kuwa singemshuku binti yangu mwenyewe anaweza nifanyie hivi, sikuamsha kengele yoyote.”

"Kama Mungu atakavyokuwa, alimpeleka mume aliyependekezwa nyumbani kwa baba yake huko kusini-mashariki, baba alidai kujua aliko mtoto wake kwanza kabla ya kushughulikia ombi lake la ndoa.”

"Baadaye alimdanganya kuwa mtoto amekufa, lakini baba alienda kwa mganga na akaambiwa mtoto yuko hai. Kisha akamtishia na akafunguka na kumwambia ukweli kwamba alikuwa akiishi na mwanamke huko Enugu.”

"Baba yake aliponiarifu, niliripoti kisa hicho kwa polisi ambao walimkamata upesi yeye na mwandani wake, mlanguzi wa watoto," mama huyo aliyefadhaika alisimulia.