Mwanamke wa miaka 39 ananguka nayo mtandaoni kutafuta mume, aahidi kufadhili harusi

“Ikiwa wewe ni msukuma mkokoteni, wewe ni omba-omba, wewe ni makanga,… tafadhali nioe, tafadhali mimi nitajitolea kufadhili kitu kila kwenye harusi. Nitakupa hadi pesa za kulipa mahari yangu." alisema.

Muhtasari

• Katika video ambayo mwanadada huyo alishiriki kwenye mitandao ya kijamii, alisema kwamba amekuwa single kwa muda mrefu na hataki kuendelea vivyo hivyo.

• Alisihi apewe mume, akisema kwamba hivi karibuni angefikia kukoma hedhi na hangependa kuwa mseja atakapoacha.

Mrembo alia kutafuta mume
Mrembo alia kutafuta mume

Mwanamke mwenye umri wa miaka 39 anachukua hatua mikononi mwake kutafuta mume na kutoa hakikisho kwamba yuko tayari kujitolea kufadhili harusi hiyo.

Mwanamke huyo alienda kwenye mitandao ya kijamii kulia na kuomboleza kuhusu hali yake ya kuwa mchumba kwa muda mrefu.

Katika video ambayo mwanadada huyo alishiriki kwenye mitandao ya kijamii, alisema kwamba amekuwa single kwa muda mrefu na hataki kuendelea vivyo hivyo.

Alisihi apewe mume, akisema kwamba hivi karibuni angefikia kukoma hedhi na hangependa kuwa mseja atakapoacha.

Katika ombi la kukata tamaa, mwanamke huyo alijitolea kufadhili harusi mwenyewe, huku akiwauliza wanaume wanaopenda kumkaribia.

“Nahitaji mume, nimechoshwa na useja. Nina umri wa miaka 39. Hivi karibuni nitaingia kwenye menopause. Tafadhali nahitaji mume katika maisha yangu. Haijalishi unafanya nini, nitakubali kuolewa na wewe,” alisema kwa sehemu.

Alizidi kusema kwamba katika umri aliofikia sasa, hana nafasi ya kuchagua, kwani yeyote bora ni mwanamume anayepumua tayari hiyo ni ithibati tosha ya kukubali kuolewa naye.

“Ikiwa wewe ni msukuma mkokoteni, wewe ni omba-omba, wewe ni makanga,… tafadhali nioe, tafadhali mimi nitajitolea kufadhili kitu kila kwenye harusi. Nitakupa hadi pesa za kulipa mahari yangu. Tafadhali njoo uniowe, nimechoka kuwa single. Ninazeeka, nahitaji mwanamume kwenye maisha yangu, nimechoka hata sipati usingizi, wote wa rika langu wameolewa na wana watoto kwenye familia zao, mimi hakuna anayetaka kunioa,” aliendelea kusema.

“Kama uko na ndugu anayehitaji mke, tafadhali niunganishe naye, sitaki kuangalia ni nini unafanya, mimi nitasimamia kila kitu. Niangalie mimi, miaka 39 bila mtoto, bila mume, haya ni maisha gani?” aliongeza.