•"Naona ndoa inakuja nakimbia, sipo tayari. Mtu mmoja ndani ya nyumba maisha yako yote? Ningechoka," alisema.
Mchekeshaji Aunty Jemimah amefichua kuwa anaogopa ndoa.
Katika mahojiano na kituo kimoja cha redio cha humu nchini, Jemimah alisema anaogopa kuamka na mtu yule yule kila siku.
"Kama kuna kitu ninaogopa maishani mbali na umaskini na njaa ni ndoa.
Naona ndoa inakuja nakimbia, sipo tayari.
Mtu mmoja ndani ya nyumba maisha yako yote? Ningechoka.
Labda siku moja nitafika huko."
Jemimah anasema alizungumza na mpenzi wake kuhusu hili
"Mimi ni mkweli sana, nilipoanza kuchumbiana naye, nilimwambia nataka kwanza nipate watoto, niwe sawa kiuchumi na alikuwa sawa.
Amekomaa sana. Ikiwa ningekutana naye kabla ningeweza kuolewa."
Jemimah alipoteza mtoto wake wa kwanza kutokana na kisukari cha ujauzito.
Alilazimika kuwa induced akiwa na wiki 35 wakati wa ujauzito wake wa pili.