"Imesumbua sana kutazama" Willy Paul akoseshwa raha na video ya 2mbili akiwa na makeup (+video)

“Naomba wanaume mtoke kwa DM yangu!! Ilikuwa ni mchezo tu,” 2mbili alilalamika

Muhtasari

•2mbili alionekana akiwa ameketi kwenye gari lake huku akijirekodi akiimba wimbo huo wa hivi majuzi wa Willy Paul.

•2mbili alidai kuwa baadhi ya wanaume walimtongozakwenye simu na akawaonya kuwa huo ulikuwa ni mchezo  tu.

Image: INSTAGRAM

Mchekeshaji Andrew Duncan Oduor almaarufu 2mbili alijiunga kufanya challenge ya wimbo wa Willy Paul ‘Life is Sweet’ lakini hatua hiyo hata hivyo imeonekana kumkosesha raha mwimbaji huyo.

Katika video aliyoichapisha kwenye ukurasa wake wa Instagram, 2mbili alionekana akiwa ameketi kwenye gari lake huku akijirekodi akiimba wimbo huo wa hivi majuzi wa Willy Paul.

Kilichowashangaza wengi ni chaguo ukarabati wa video yake ambapo alitumia filter ambayo ilionyesha kama uso wake una vipodozi.

“MAISHA NI TAMU haswa nikiblock mtu wako kutoka kwenye Dms Zangu,” 2mbili aliandika chini ya video hiyo.

Pamoja na uso wenye vipodozi, mchekeshaji huyo pia alionekana akitikisa kichwa na kuusogeza mwili wake kwa majivuno kama ya kike.

Wanamtandao wengi akiwemo mwimbaji wa wimbo aliokuwa akifanyia challenge, Willy Paul, wameipokea video hiyo kwa hisia mseto.

Katika jibu lake, Pozee aliweka wazi kuwa hakuwa na raha hata kidogo wakati akiitazama video hiyo. Hata hivyo alimpongeza kwa kufanya challenge hiyo.

"@2mbili Hii ilisumbua sana kuitazama. Hata hivyo, Life is Sweet,” Willy Paul alisema.

Huku akimjibu mwimbaji huyo wa zamani wa nyimbo za injili, 2mbili alidai kuwa baadhi ya wanaume walikuwa washaanza kumtongozakwenye simu na akawaonya kuwa huo ulikuwa ni mchezo  tu.

“Naomba wanaume mtoke kwa DM yangu!! Ilikuwa ni mchezo tu,” alijibu.

Tazama maoni ya watumiaji wengine wa mtandao-

Jewelbutto: Tumbili amekuwa tumbafu nkt!

Trapkiddo_official: Lips ni za Tanasha Donna

Dimanmkareclasic: Choku alianza hivyo

Kid_dope_coyotte: Mmeanza kuonyesha true colors

Rapidkizzkaraine: Mikono tu hujapaka mafuta.

Kenyan_maina: Tumepoteza kijana yetu.