Zari awashambulia vikali wanaume baada ya kuzozana na mumewe, Shakib

Kulingana naye, wakati wanaume wanashughulika kukanyaga nje ya ndoa na uhusiano wao, wanawake wanazingatia kutafuta pesa.

Muhtasari

•Zari amewashambulia wanaume moja kwa moja, siku chache tu baada ya kutofautiana hadharani na mumewe, Shakib Cham.

•"Kuwa na kiti, hatuwezi kuwa sawa," alisema.

Image: INSTAGRAM// SHAKIB CHAM

Sosholaiti na mjasiriamali maarufu wa Uganda,  Zari Hassan amewashambulia wanaume moja kwa moja, siku chache tu baada ya kutofautiana hadharani na mumewe, Shakib Cham Lutaaya.

Katika taarifa fupi aliyoitoa kwenye Instagram siku ya Ijumaa, mama huyo wa watoto watano aliwashutumu wanaume kwa kuzingatia kuwa na familia za siri bila ufahamu wa wapenzi wao.

Kulingana naye, wakati wanaume wanashughulika na kukanyaga nje ya ndoa na uhusiano wao, wanawake wanazingatia kutafuta pesa.

"Wanawake wanawekeza kwa siri huku wanaume wakitengeneza familia za siri," Zari alidai.

Alibainisha kuwa jambo hili l inawafanya wanawake na wanaume kutokuwa kwenye kiwango sawa.

"Kuwa na kiti, hatuwezi kuwa sawa," alisema.

Haijabainika ikiwa ujumbe huo una uhusiano wowote na matukio ya hivi majuzi katika ndoa ya sosholaiti huyo mwenye umri wa miaka 43 au ni nini kilimchochea kufanya chapisho hilo.

Ziara ya hivi majuzi ya mwimbaji Diamond Platnumz kwa Zari na familia yake nchini Afrika Kusini ilionekana kuleta matatizo katika ndoa ya sosholaiti huyo.

Takriban wiki mbili zilizopita, Zari alizamia kwenye mitandao ya kijamii kumzomea mumewe Shakib na kutishia kumuacha. Hii ilikuwa baada ya Shakib kuonyesha kutilia shaka uhusiano wa  Diamond na mkewe.

Katika kipindi cha moja kwa moja kwenye mtandao wa kijamii, mama huyo wa watoto watano alifichua kuwa mumewe hana uhakika kuhusu ndoa yao na amekuwa akihoji uhusiano kati yake na mzazi mwenzake, Diamond Platnumz.

Zari alisema alilazimika kufanya kipindi cha moja kwa moja ili kueleza wazi kuwa yeye na Diamond hawako kwenye uhusiano wowote wa kimapenzi, ili tu kumhakikishia mumewe kuhusu auaminifu wake katika ndoa yao

“Ngoja niwaambie kitu, Nikitaka kumrudia Diamond naweza kurudi. Ikiwa Diamond anataka kunirudia, anaweza kurudi. Lakini sisi tumemalizana. Sisi tumemalizana kabisa. Simtaki, hanitaki,” Zari alisema Jumapili usiku.

Sosholaiti huyo aliweka wazi kuwa ana mume na mzazi mwenzake pia ana mpenzi.

“Mume wangu hajiamini sana, na hilo linaleta matatizo mengi. Lazima niwe hapa kuelezea. Kweli? Boss lady mzima, inabidi nifanye kipindi chote cha moja kwa moja, ili tu kuthibitisha uhakika kwa mume wangu. Kipindi hiki ni kuthibitisha kitu kwa mume wangu,” aliongeza.

Mfanyabiashara huyo mwenye umri wa miaka 43 alibainisha kuwa ana sifa zote nzuri na anaweza kuwa na mtu yeyote ambaye anataka kuwa naye.

"Lakini nilimchagua mume wangu, na sijali jinsi nyinyi mnamwona. Ooh, amefilisika, hafai vya kutosha, sijali. Nilimchagua. Nilichagua kuwa naye kama mume wangu, kisha ananiweka katika hili!!,” alisema.

Zari alidokeza kuwa mumewe hana budi kuacha kutokuwa na uhakika kuhusu ndoa yao ikiwa anataka iendelee vyema.